WanaJF,
Baada ya kufanikiwa katika maandalizi ya kilimo sasa nimefikia kubuni biashara sambamba na kilimo. Katika harakati za kutafuta biashara ya kufanya nimefikia uamuzi wa kuanzisha biashara ifuatayo:
(i) Nguo za watoto kati ya 0-12yrs na mahitaji yao mengine lakini pia nikijumuisha pamoja baadhi ya mahitaji ya akina mama.
(i) Simu za mikononi na makasha yake.
Hii yote itakuwa katika mkoa wa Mwanza.
Ombi langu kwa wale wenye uzoefu na hii biashara ni kwamba naomba kupata connection na wafanyabiashara wa jumla wa nguo za watoto hapa Tanzania especially Kariakoo lakini pia ninaomba kufahamishwa ni nchi zipi wafanyabiashara wa nguo wa Tanzania wanachukulia nguo zao kwa jumla. Hapa namaanisha nguo ambazo ni affordable kwa watanzania wenye kipato cha kati na cha chini.
Naomba pia nifahamishwe ni nchi gani wafanyabiashara wa simu za mikononi wanapata hii bidhaa. Nilisikia kuwa kuna nchi simu zinauzwa katika mzani na akina mama wa Uganda wanaenda sana huko, je kuna mtu mwenye data za hii biashara? maana zamani ilikuwa dubai lakini siku hizi nasikia dubai hailipi tena. Naomba msaada kwa wazoefu wa hii kazi.
Ushauri katika hii biashara pia utakuwa mhimu sana.