Msaada: CYLINDER HEAD ya COASTER/LAND CRUISER - 1HZ

Msaada: CYLINDER HEAD ya COASTER/LAND CRUISER - 1HZ

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,762
Reaction score
2,196
Wadau,

Gari yangu (Toyota Coaster) imezingua Cylinder head, inachemsha mno na kila nikiijazia/nikiziba matundu inakatika tena. Ikitoka Mwenge - Posta lazima iwekwe maji, na ikitoka Posta - Mwenge pia lazima iwekwe maji tena. Nimefikiria nijipange tu ninunue Cylinder head ingine tu, kuna mdau yeyote mwenye taarifa ya wapi nitapata hii kitu kwa urahisi kwa maduka ya hapa Dsm? Used/Mpya?

Kuna jamaa kaniambia nijaribu kucheki kwenye google kwa nchi za Japan, Dubai au China mfano Cylinder Head 1hz 11101-17012 Factory,Cylinder Head Baretoyota Coaster/land Cruiser 4164cc 4.2d+td - Buy Cylinder Head 1hz,Cylinder Head 11101-17012,Cylinder Head Coaster/land Cruiser 4164cc 4. Product on Alibaba.com, sasa sijajua napo cost zake ukiweka na kodi inakua ngapi. Mdau yeyote mwenye taarifa pia kwenye importation ya hizi vitu msaada please, Maana gari yenyewe ni ya Biashara, so ikilala siku kadhaa tu hasara.

Msaada please!!
 
Umeisha pata kama bado ni pm niingie chimbo na offer yako!!
 
Ilala baada ya machinga complex ukitokea magomeni kata kushoto kama unaenda shaurimoyo upande wa kulia nyumba ya kwanza au ya pili uilizia Kilonja, West au Muddy.

Ukiwakosa hao zunguka mtaa wa Songea kuna mtu anaitwa White, Casto au Ingia Duka lolote lenye jina Mkweche then Ulizia Chopa!!!!

Ukikwama PM
 
Mkuu,
Nimekupata, na ahsante sana!!
Pia cheki PM
 
Mkuu hzo zipo nyingiii kama dsm hakna mikoa ya arusha na moshi zipo mana kule zinatumika sana hzo gari na pia zipo zilizopata ajali nyingi so kupata spare ni rahisi

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kaka gari yako ni model gani(mwaka gani)nawezakukutumia bila tatizo lolote
 
Mkuu hzo zipo nyingiii kama dsm hakna mikoa ya arusha na moshi zipo mana kule zinatumika sana hzo gari na pia zipo zilizopata ajali nyingi so kupata spare ni rahisi

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Ahsante Mkuu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom