ushauli ni mzuri kiongozi siyo kila kitu lazima uende hospital sababu kuna watu wanaweza wakawa na njia mbadala lakini pia kumbuka niko mbali sana hospital
Ikiwa kemikali kama vile asidi au alkali, mate ya nyoka, saruji (cement), chokaa au cheche ya moto vimeingia kwenye jicho, jambo la kwanza ni kuchukua chombo chenye maji safi kisha zamisha macho yako kwenye maji hayo safi kwa kutazama ndani ya maji huku ukiyaosha, unaweza kuendelea na zoezi hili kwa dakika 15, pia unaweza kutumia njia hiyo kama umeingiwa na mchanga au kitu chochote machoni. Ikiwa kope zimeteketezwa kwa kuungua au kuharibika, tia mafuta ya macho ya ''tetracycline'' kisha fika haraka hospitali.
Unaweza kutumia maji safi ya kawaida au maji ya drip (normal saline)