Msaada chakula bora kwa mtoto mdogo wa miezi 4.

Access Denied

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Posts
655
Reaction score
211
Wana jamvi naombeni kuuliza ni chakula gani bora naweza kumpatia mtoto wa miezi 4 na hata jinsi ya kuvichanganya maana najua vinakua katika mfumo wa uji.
 
Miezi minne bado, subiria mpaka afikishe miezi sita akiwa ananyonya maziwa ya mama tuu endapo afya ya mama inaruhusu na kama maziwa yanatoka. Maana maziwa ya mama yana virutubisho vyote ambavyo unavitaka sasa, pia uwezo wa mfumo wa mmeng'enyo wa mtoto na utumbo bado havijakomaa, subiria vikomae, then aje aanze na uji wa kawaida ambao ni laini sana na maziwa ya ng'ombe au mbuzi, akifikisha miezi nane, unaweza kumsagia uji wa lishe wenye mchanganyiko wa vitu vingi kama ulezi/mtama, karanga, mahindi, maharage/kunde/njegere, mchele, na wakati wa kupika unaweka maziwa na baadaye unaweza kuanza kumtengenezea mtori, na juisi ya matunda mchanganyiko kwa sana. Kila la kheri kwenye malezi bora ya mtoto, na jitahidi sana maana wanahitaji uangalizi wa karibu sana.
 
Ahsante sana mkuu.
 
Inategemea, daktari alishauri kuanza kumpa mwanangu chakula kilichosagwa ( puréed ) kuanzia miezi mitatu aina ya cereal. Either rice cereal au oatmeal. miezi minne unaweza kuanza na ndizi, avocado, carrot, viazi vitamu, na green peas. Zote Zoe zimesagwa kuwa Kama mtori na blender. onana na daktari wa mtoto wako kwa ushauri zaidi.
 
miezi 4,viazi mviringo unachanya na carrot unasaga na blenda.au viazi,peas,carrot na supu ya kuku,unasaga vinakuwa laini.au baby cerial ya mchanganyo wowote ule.uji mlaini.na maziwa ya mama kwa wingi.muanzie kidogo kidogo.au unamsagia mchanganyiko wa vegetables,ila viwe laini
 
Ahsante sana mkuu.

Karibu sana mkuu kwenye malezi. Ila kama kuna tatizo au maziwa ya mama hayamtoshi, may be analia sana nenda kwa daktari kwa ushauri zaidi. Lakini kama yupo vizuri na hasumbui maziwa ya mama ni tosha mpaka afikishe miezi sita. Ila mama ajitahidi sana kula diet na vyakula vya kuongeza maziwa ya mtoto.
 
Mie sikuwa na maziwa hivyo akiwa na umri wa miezi 4 nilimwanzishia mtoro,kaugali lainii sana na mchuzi mzito wa maharage.
Na maziwa hivyo hivyo.Namshukuru Mungu kanikuzia mtoto bila tatizo lolote na sasa ana miaka 3.na kichwani yupo njemaa sana kanasoma.
 
Karibu sana mkuu kwenye malezi. Ila kama kuna tatizo au maziwa ya mama hayamtoshi, may be analia sana nenda kwa daktari kwa ushauri zaidi. Lakini kama yupo vizuri na hasumbui maziwa ya mama ni tosha mpaka afikishe miezi sita. Ila mama ajitahidi sana kula diet na vyakula vya kuongeza maziwa ya mtoto.

Kiukweli mtoto hua hatosheki na maziwa ya mama yake maana hua analia sana.
 
miezi 4,viazi mviringo unachanya na carrot unasaga na blenda.au viazi,peas,carrot na supu ya kuku,unasaga vinakuwa laini.au baby cerial ya mchanganyo wowote ule.uji mlaini.na maziwa ya mama kwa wingi.muanzie kidogo kidogo.au unamsagia mchanganyiko wa vegetables,ila viwe laini

Hivi vitu unavichanganya baada au kabla ya kupika?
 
Kiukweli mtoto hua hatosheki na maziwa ya mama yake maana hua analia sana.

Huyo anaweza kuanza kwa mchanganyiko kawa ulivyoshauriwa hapo juu. Vyote ni vema ukivisaga kabla ya kuvipika. Mimi wa kwangu amezaliwa june 2012 na amenyonya maziwa ya mama tuu mpaka december, ndo alianza uji laini na vitu vingine laini sana, then sasa hivi ndo amesagiwa lishe yenye mchanganyiko wa vitu vingi sana na maziwa ya ng'ombe. Lakini wa kwangu alikuwa hasumbui wala halii na mama yake maziwa yalikuwa yanatoka sana na kulikuwa na ratiba maalumu ya kumnyonyesha na ilikuwa ikizingatiwa.
 
Si shauri sana kumpa artificial food,pmikie kama kisukari anavosema na kajuice kidogo ,ndizi unachanganya na viazi una blende kauji kidogo ila unga uchujwe usimpe mwingi ataota kitambi njaaa,kidogokidogo,usimlishe mtoto artificiaal food ni mbaya sana eti serilac maziwa ya makopo mhhhhh
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom