Wakuu, nina Apple IPhone 4S. Naona toka jana nikichaji baada ya kuchomoa tu chaji inaniambia "battery low, shutting down". Nahisi battery imekufa kwani wakati wa kuchaji inaonyesha chaji inaingia hadi asilimia 100. Sasa kwa mwenye battery mpya tuwasiliane PM akitaja bei na gharama za kufunga. Awe DSM tafadhari maeneo ya katikati ya jiji ili iwe rahisi kwangu kumpata.
battery ya iphone 4s dar utaumia, ni zaidi ya laki. kama imetokea ghafla tu huenda tatizo siyo battery, jaribu kutumia charger nyingine (original), wakati mwingine huwa zinazingua, ukiona bado jaribu kufanya hard reset. ukiona bado agiza battery ebay, kkufunga unafunga mwenyewe (labda kama ni mwanamke au mzee ndiyo utashindwa)
Nimejaribu kufuatilia naona inatatizo jingine tu kwani inajizima,kisha baada ya masaa machache ukiiwasha inawaka tena na kuendelea kufanya kazi kama kawaida. Nimepitia setting zote naona zipo kawaida tu. Nadhani inanipa dalili ya kuanza kutafuta simu nyingine. Hiyo hard reset haikubali.
iPhone huwa haifi kirahisi mkuu. Hard reset haikubali vipi mkuu? nina imani ukiirudisha factory default itarudi kuwa mpya. umeinstall iOS version gani?
Or format yote,kutakua na apps inayodrain battery.reset ya factory just try it.