Pablo Blanco
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 7,328
- 6,591
unafuga nini now??Hapana mkuu niliwahi fuga wakanizingua ugonjwa wa ndui nikaachana nao!
unafuga nini now??Hapana mkuu niliwahi fuga wakanizingua ugonjwa wa ndui nikaachana nao!
mayai vipi??? nyama ya bata ipoje??Bata mkuu
View attachment 1244562
Wa kawaida kwa ajili ya mahitaji binafsi ya nyama mkuu sio kwa biashara!
Kwa mwenye kujuwa huu ugonjwa, tafadhali anisaidie niwape dawa gani wana zunguka zunguka kwa kukunja shingo mwisho wana kufa View attachment 1229717
mia mzee,umetishaaaaaView attachment 1244844
Bonge la nyama
Ukiwapa pumba usichanganye na maji weka maji pembeni na pumba pembeni.Kwa mwenye kujuwa huu ugonjwa, tafadhali anisaidie niwape dawa gani wana zunguka zunguka kwa kukunja shingo mwisho wana kufa View attachment 1229717
Shukran mkuu waliuguwa 2 mmoja akafa walikuwa wa kubwa ninao zaidi ya 60Pole sana kiongozi, japo nimechelewa kuona uzi huu ila naimani mchango wangu utakua na manufaa hata kwa siku zijazo.
Nimesoma maoni ya wadau wengi wakizungumzia upungufu wa madini Calcium na Phosphorous yanayopatikana kwenye Chokaa na Unga wa mifupa kwa wingi (Upungufu wa viini lishi hivyo haviwezi kuleta madhara yenye kuonesha dalili hizo mpaka kupelekea kifo cha bata vifaranga) Bali kuna mambo mawili niliyonayo hakika yanaweza kuleta athari zenye dalili hizo tajwa na mleta uzi
Mosi: Upungufu wa madini aina ya Selenium(Se) na Vitamin E (Huathiri kundi dogo na vifo huchukua muda kutoa, maana wanakua kama mgonjwa wa kifafa(Seizure), kinamshika atarukaruka,kujipiga chini baadae kinamuachie na anakua kawaida.
Pili: Ugonjwa hasa wa Virusi ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama Duck Viral Hepatitis (DVH), Ugonjwa huu ni hatari ni kama Kideri/Mdondo kwa kuku, huwapata Vifaranga wa bata Wasiozidi Umri wa wiki 6, mara chache sana wiki 8.
Vifo ni vya haraka sana mara dalili zinapojionesha.
Dalili kuu ni kujipigapiga chini huku amekunja shingo, kurusha rusha/kunyoosha mabawa na miguu(Kifafa)
Vifo huweza kufikia asilimia 100 ndani ya siku chache tangu dalili kuonekana Japokua kupona kunawezekana ila sio kwamba kuna dawa, TIBA MBADALA (SUPORTIVE TREATMENT YAWEZA KUMNASUA KWENYE MIKONO YA ISRAELI JAPO SIO GUARANTEE)
Mazingira machafu ni chanzo kikuu cha maambukizi kwa vifaranga.
Ugonjwa huu HAUNA DAWA BALI HUKINGWA KWA CHANJO ambayo bata hupatiwa na umri wa siku moja, Usafi wa sehemu ya kulalia(Kiota/kiatamizi) na mazingira wanayoshindia vifaranga.
Tambua huu ni ugonjwa wa vifaranga walioko chini ya 8.
Kama utaweza wape chanjo ya Kideri/Newcastle wakubwa kwa wadogoShukran mkuu waliuguwa 2 mmoja akafa walikuwa wa kubwa ninao zaidi ya 60
Vifaranga ninavyo vingi Ila sija vichanganya
Walio uguwa walikuwa wanakosa nguvu miguu shingo wana kunja kama ulivyo sema!
Sijawahi wa chanja chanjo yoyote una shauri ni wape chanjo hawa wakubwa tu au wadogo?
Msaada Mkuu, nimetotolesha jana.magonjwa ya Bata wakubwa nami hunitesa, hasa ya kushindwa kusimama. Ukitotolesha wadogo tuwasiiane, dawa ipo nitakuelekeza bure.
Samahani mkuu! Hii chanjo ya kideri. Newcastle ukiwapa vifaranga wa batae itawaokoa hao Vifaranga kutoka ktk kifo? Au ni kama kubahatisha tu?Kama utaweza wape chanjo ya Kideri/Newcastle wakubwa kwa wadogo