Msaada: Baharia Mtanzania amefia Iran

Lavan Island

JF-Expert Member
Oct 24, 2015
2,377
2,048
Habari za jioni wana Jf,

Nimepewa taarifa na rafiki mmoja hivi anaomba msaada wa kibalozi.
Ishu ipo hivi kuna baharia mwenzao alisafiri kwa meli kutoka Dubai kwenda Iran bahati mbaya alipata ajali akiwa kazini yani alianguka akaumia kichwani alipelekwa hospitali bahati mbaya sana aliumia vibaya kiasi cha ubongo kuchanganyika na damu na finaly akafariki akiwa hospitali.Na Mpaka sasa ni 10 days kampuni yake imekaa kimya.

na meli imetembea kuelekea nchi nyingine. Je kuna ubalozi wa Tanzania kule Irani ni sehem gani labda anaweza kumfuatilia ili haki za huyu mtu zipatikane,wamejaribu ku mtaarifu balozi wa Tanzania Dubai isipokuwa hawaoni jitihada zozote mpaka sasa,

Tunaomba ushirikiano wenu.
 
mkuu pole...km unawafaham ndugu na jamaa zake wakaribu wasiliana nao haraka..ili waweze kuongea na serikali yetu hapa nchi..kisha wafanye utaratibu wa kuuleta mwili wa mtanzania mwenzetu.
 
Jaribu kuwasiliana Na ndugu zake wawasiliane Na wiraza ya mambo ya nje wanaweza wakapata msaada
 
Jaribu kuwasiliana Na ndugu zake wawasiliane Na wiraza ya mambo ya nje wanaweza wakapata msaada
Taarifa wanazo ispokuwa jinsi ya kuuleta huo mwili wa marehm hapa Tz ndio inshu kubwa kwa sasa.Na pia haki za huyu mtu je?
 
mkuu pole...km unawafaham ndugu na jamaa zake wakaribu wasiliana nao haraka..ili waweze kuongea na serikali yetu hapa nchi..kisha wafanye utaratibu wa kuuleta mwili wa mtanzania mwenzetu.
Ndio ndugu wamesha pewa taarifa kuna sehem wamekwama.
 
Tuliza akili Mkuu hili suala ni muhimu kuliko unavyofikiri,kwanza eleza vizuri alikuwa anafanya kazi na kampuni gani ya Meli toka Dubai toa e mail yao alafu wahusika wafanye mawasiliano nao kujua utaratibu wa kuweza kusafirisha huo mwili toka Irani mpaka Tanzania mambo ya haki zake itakuwa baadae taratibu zipo wala haki zake haziwezi kupotea kulingana na mkataba wake unavyoeleza.
 
Nadhani anachodai mwandishi cha kwanza ni kwa kampuni husika kuusafirisha mwili kuurudisha kwao, sio familia ianze kuomba omba utadhani ndugu yao alikuwa mzurulaji tu huko iran. Hivyo anaye weza kumsaidia namna ya kuiwajibisha hiyo meli isafirishe meli na kutoa stahiki nyingine afanye hivyo. Sio kutoa maneno ya shombo, hayasaidii.
 
Well said man!wengi humu kila kitu wanafanya mzaha
 
Huyu Mtu anasiku 10 hospitalini tangu apoteze uhai wenyewe wanadai cost ni kubwa almost dola 15 ku release ule mwili uletwe africa kampuni ya marehem iliyo mwajiri nayo wanasema aliajiriwa kupitia ajent,ambae keshatafutwa na taarifa anazo ila simu mpaka usawa huu imezimwa.
 
mkuu toa jina la kampuni aliokua anafanya kazi...melini ni sehemu ambayo haki huwa haipotei na gharama pia za matibabu au kurudisha mwili wa marehemu zipo juu yao...toa jina tujue imesajiliwa wapi ili ubalozi ushughulikie iyo sehemu iliyosajiliwa kampuni na so sehemu waliopatia ajira kama kuna utata...
 
kama ana undugu na JECHA wa ZANZIBAR shauri yake ila kama hawana undugu naomba Ubalozi wetu riyadh saudi arabia umsaidie kufuatilia haki na stahili zake
 
mkuu pole...km unawafaham ndugu na jamaa zake wakaribu wasiliana nao haraka..ili waweze kuongea na serikali yetu hapa nchi..kisha wafanye utaratibu wa kuuleta mwili wa mtanzania mwenzetu.
Hiyo haitasaidia anachotakiwa aongee na ubalozi wa Tanzania nchini Iran ni hao tu ndo wataweza kumsaidia.
 
wewe haki zake zinakuhusu nini .mwili kwanza haki ndugu zake watafuatilia
Haki zake ni kwamba kisheria kampuni inapaswa kuusafirisha mwili kwasabab jamaa ameumia kazini, usiwaze kiinua mgongo tu, hapo kampni inapaswa imlete baba au mama aende iran ua Dubai wakabidhi haki za marehemu na mwili. hiyo kampuni haiwezi fanya hayo mpaka apatikane mtu wa ubalozini afatilie kwa karib.
 
Hata mimi nikaanza kuhisi labda shida ni haki, mwili hawahitaji. Wameshindwa hata kwenda foreign wanataka haki kwanza!!!
Haki ni pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu, kisheria kampuni inapaswa kuusafirisha mwili na kawaida inabidi baba au mama yake au kaka yake wa tumbo moja mwenye passport jina moja aende ndo atapewa mwili wa marehemu, hiyo kampuni magumashi ndo tatizo na ubalozini ukifatilia ndo jamaa atapata hizo haki zinazosemwa.
 
kama ana undugu na JECHA wa ZANZIBAR shauri yake ila kama hawana undugu naomba Ubalozi wetu riyadh saudi arabia umsaidie kufuatilia haki na stahili zake
Hivi wewe kabla ya kupost umesoma hiyo comment yako??? mambo ya jecha yanakujaje hapa????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom