Msaada: Anayejua comprehensive motor insurance

nataka kujua

Member
Joined
May 1, 2014
Posts
31
Reaction score
5
nimatumaini yangu wana jf wazima ninaomba msaada kwa anayefahamu kuhusu comprehensive motor insurence anieleze kiundani
 
nimatumaini yangu wana jf wazima ninaomba msaada kwa anayegffahamu kuhusu comprehensive motor insurence anieleze kiundani

Ntaeleza kwa kifupi sana.
Kuna insurance okikata, ukipata ajali haulipwi/haufidiwi wewe mwenye gari bali anafidiwa uliyemsababishia ajali tuu na pia gari ikiungua pia haulipwi/haufidiwi.

kuna nyingine ukipata ajali haulipwi labda uwe umesababishiwa ajali na ithibitishwe na mahakama lakini ukipata ajali ya moto haulipwi.

Kuna insurance nyingine ukipata ajali haulipwi wewe mwenye gari bali analipwa uliyemsababishia ajali tuu lakini gari yako ikipata ajali ya moto/ikiuungua unalipwa.

Na kuna insurance nyingine ukikata, inakava kila kitu yaani ukipata ajali ajali usababishe wewe au usisababishe, gari ikipata ajali ya moto Unafidiwa. hii ya mwisho inayokava kila kitu ndiyo inaitwa COMPREHENSIVE.

Bila shaka nimjitahidi kukuelewesha angalau umepata picha.
Otherwise majibu yoote hayo ungeyapata kiulaiini kama ungetumia GOOGLE.
 
nimatumaini yangu wana jf wazima ninaomba msaada kwa anayefahamu kuhusu comprehensive motor insurence anieleze kiundani

Mkuu kuna aina tatu za motor insurance
-THIRD PARTY ONLY.Hii ni lazima gari lako liwe nayo kwa mujibu sheria ya nchi,hii policy inamcover mtu wa tatu i.e third party ambaye hayuko kwenye mkataba kati yako Insured na Kampuni ya bima Insurer.Sasa basi ikiwa gari lako/pkpk ikikonga na kuharibu gari lingine,kumgonga mtu na kumsababishia majeraha au kifo au likiharibu mtu mwingine hii policy itakusaidia kulipa lkn tambua bima hii hailindi gari lako ni third party tu.

-THIRD PARTY FIRE & THEFT,Hii policy inafanya kazi kama hiyo ya kwanza na ziada,ikiwa gari lako litapata uharibifu kutokana na moto na kuibiwa au jaribu la kuibiwa,ni nzuri ukiwa nayo lkn siyo bora.

COMPREHENSIVE.Hii ndio bima kubwa kwa vyombo vya moto sababu inajumuisha hizo policy zote na zaidi inalilinda gari lako ikiwa litaharibika kutokana na ajali,ukiwa na hii policy you are on safe side coz imekava risks zote.Na hata gharama yake ni kubwa kulinganisha na izo zingine.Hope umepata mwanga kidogo.
 
Ni sawa kabisa ila kwa maelekezo ya ziada wasiliana na MAENDELEO benki kwa namba 0658 500420 niliwasikia wakijinadi hivyo kuwa siku hizi wanatoa huduma hiyo.
 
Back
Top Bottom