Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Habari wana wakubwa

Kwa kweni nakuja mbele yenu kutaka msaada niko na mke wangu mwaka wa 8 sasa na tumebahatika kupata watoto 2 wa kike na wa kiume.

Kwa hakika nampenda sana mke wangu kwani tumetoka mbali alinivumilia kuishi na mm kipindi kigumu cha kipato changu kua pia kwa kunizalia watoto.

Shida ni kua mke wangu kila siku tunakwaruzana kisa simu akiona simu inapigwa yeye ataikimbilia akiona jina la mwanamke basi anaweza kuipokea ili ajuwe ni nani au anataka musikilize shirika ukimalize aanze kuhoji huyo ni nani na anatala nn? Ukimiambia kua ni rafiki hakuelewi hapo ataanza oooo unawana wake kwa kua siku hizi una kazi kila nikijitahidi kumuelewesha basi hakubali ananiona kicheche

Hadi naiona ndoa haina amani mpaka natamani hata kutoa maamuzi mabaya ila tatizo watoto wangu bado wadogo nimekua namchoka kwa kutokuniamini hadi maneno machafu yanamyoka hutamani kumpiga ila najihisi nitamuonea.

Mimi simu yake sishiki wala sifuatiliii maana sioni sababu na nimemnunulia simu mbili ila anaweza akazifungia hata wiki eti hazina chaji wakati nyumbani pana umeme namtilia salio kwa mwezi basi unaweza kuisha mwezi bila ya yeye kutumia hilo salio.

Kwa kweli nampenda sana ila kuacha kutumia simu kwa ajili yake siko tayari kwani kazini kwangu kia na simu ni jamabo la lazima .
 
ndio ndoa hizo jamaa yangu, enewei yahitaji kuwa mvulivu hilo suala ni kupita, ni kipindi cha mpita japo ni kigumu, yawapaswa kukaa na kuongea kwa ukaribu zaidi....
ila jitahidi kuwa muwazi kwake, kama unahisi tatizo kuwa mpole muache apokee simu....
 
alishawahi kukuta sms mbaya kwenye simu yako ?au kukufumania? au kukukuta na msichana mazingira ya kutatanisha? majibu ya hayo ndio yatatoa mwanga mzuri
 
Du pole sana ....wivu uo mara nyingi una tokea katika ndoa....ila jarb kumu elewesha
 
We muachie tu aendelee kuzipokea baadaye akisha gundua kuwa hakuna hila ndani yako ataacha mwenyewe tu hata ikiita atakuwa anakuletea upokee mwenyewe...ni swala la muda tu......"Mungu ameumba jambo jipya duniani Mwanamke atamlinda mmewe"
 
Inategemea labda ulishampa reason ya kuku doubt, kuna wanawake tuko hivyo yani nikikumaini nakuamini kweli ila ukinipa sababu ya kutokukuamini kweli utajuta, haiwezekani ndani ya miaka 8 muishi vzr bila hizo kelele leo from no where aanze visa, ingekuwa umesema kwamba ulipomuoa ulikuwa na pesa lakini kwasasa hali mbaya ningeweza sema anatafuta sababu baada ya kuonamambo yamekuwa magumu lakini kama alionyesha upendo wa kweli kipindi cha dhiki iweje kwenye neema ndo aanze visa? hapana bwana kuna namna, tuelezee vzr
 
maswala mtambuka haya, inaonekana mkeo anakupenda kuliko unavyompenda na unaonekana hujalitambua hili. Kwa kuwa wewe ni mwaminifu kwenye ndoa yako basi mkubalie apokee simu zako zote unazopigiwa ukiwa naye mpaka aridhike kuwa hauwindwi kwenye simu.

Ni maswala Mtambuka haya, jipime uadilifu wako.
 
Kwa mtindo huu inaelekea ulianza tabia za kumfanya mkeo awe ana ku doubt!!! Kama haikuwepo zamani basi jichunguze na jibu utalipata!!!! Hizi simu za mkononi zimerahisisha sana mawasiliano ila ni majanga kwa mahusiano mengi mno, tena mengine yamevunjika irreparable.
 
Kama huna michepuko we pokea tu na kuongea na hao wanaokupigia simu kama hamna jambo baya mnalozungumza akisikia kuna shida gani?
Kama una mambo yasiyofaa ambayo unazungumza kwenye simu acha udumishe ndoa yako kama ndoa haina tatizo jingine kweli unawaza kuachana na mama watoto sababu ya simu tena unazopigiwa wewe?!
Hayo ndo maisha ya ndoa mkuu lazima kuna vitu utoe sadaka(vi-sacrifice).
 
Pole ndugu. Tumeambiwa tuishi nao kwa ajili sana hawa watu. Wewe ni mwanaume inabidi utumie akili sana usikurupuke na kutoa uamuzi wowote mbaya, hakuna alie msafi ndugu yangu, ukiona umeongea nae ila bado hajakuelewa jaribu kumshirikisha mtu wake wa karibu kama dada yake, unaweza kupata jibu....
 
We muachie tu aendelee kuzipokea baadaye akisha gundua kuwa hakuna hila ndani yako ataacha mwenyewe tu hata ikiita atakuwa anakuletea upokee mwenyewe...ni swala la muda tu......"Mungu ameumba jambo jipya duniani Mwanamke atamlinda mmewe"

Ni kweli! Kama simu hazina tatizo amuache tu aendelee kupokea na kutoa maelezo yanayojitosheleza!
 
Tatizo si kupokea simu za mumewe wakati mwingine anamwuliza maswali mengine huyo mpigaji Hali hajui man uhusiano gani. Wakati mwingine ni mtu anayekuletea dili sasa akiulizwa first time Mara nyingine atakuletea dili kweli.

Mwisho wa siku mnawafanya Wanaume kuonekana Kama wanatawaliwa ndani ya nyumba.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwache apokee tu..ili aridhike.sasa akipokea atakua na cha kuongeanae huyo mtu wa upande wa pili?
 
Habari wana wakubwa

Kwa kweni nakuja mbele yenu kutaka msaada niko na mke wangu mwaka wa 8 sasa na tumebahatika kupata watoto 2 wa kike na wa kiume.

Kwa hakika nampenda sana mke wangu kwani tumetoka mbali alinivumilia kuishi na mm kipindi kigumu cha kipato changu kua pia kwa kunizalia watoto.

Shida ni kua mke wangu kila siku tunakwaruzana kisa simu akiona simu inapigwa yeye ataikimbilia akiona jina la mwanamke basi anaweza kuipokea ili ajuwe ni nani au anataka musikilize shirika ukimalize aanze kuhoji huyo ni nani na anatala nn? Ukimiambia kua ni rafiki hakuelewi hapo ataanza oooo unawana wake kwa kua siku hizi una kazi kila nikijitahidi kumuelewesha basi hakubali ananiona kicheche

Hadi naiona ndoa haina amani mpaka natamani hata kutoa maamuzi mabaya ila tatizo watoto wangu bado wadogo nimekua namchoka kwa kutokuniamini hadi maneno machafu yanamyoka hutamani kumpiga ila najihisi nitamuonea.

Mimi simu yake sishiki wala sifuatiliii maana sioni sababu na nimemnunulia simu mbili ila anaweza akazifungia hata wiki eti hazina chaji wakati nyumbani pana umeme namtilia salio kwa mwezi basi unaweza kuisha mwezi bila ya yeye kutumia hilo salio.

Kwa kweli nampenda sana ila kuacha kutumia simu kwa ajili yake siko tayari kwani kazini kwangu kia na simu ni jamabo la lazima .

Stress za kushinda home hizo, mtafutie shughuli ya kufanya!! Mfungulie hata kaduka mitaa hiyo hiyo ya home kamuweke busy utaona yote hayo yataisha!!
 
kama una hakika we si kicheche na wala hujawahi kumpa sababu ya kutokukuamini basi tatizo ni yeye, ni "possessive". hangaika kaka kwani mwisho kabisa kama mtashindwa kuaminiana hiyo ndoa itakufa kifo cha mende; mtabaki ndani ya nyumba kulea watoto. Sasa wewe punguza hasira ingawa inaudhi. Tafuta siku ambayo wewe na yeye mna raha zenu, tokeni wawili ila msikae kwenye kificho sana anza kutoa yaliyo moyoni mwako; mwambie jinsi tabia yake (na siyo yeye) inavyokuathiri na inavyoathiri ndoa yenu na unavyoona inakoelekea. Mweleze umuhimu wa kujichanganya na watu wengine (ndugu, jamaa na marafiki), kitu ambacho na yeye pia anatakiwa kukifanya. Mwambie unampenda kuliko hao wengine ila na wenyewe wana nafasi zao kwenye maisha yenu.

Halafu tabia yake/mahusiano yake na watu wengine ikoje? Ana furaha ukiwa na ndugu na jamaa zako? Na je ana kazi ya kufanya? Ukishindwa kabisa kutatua mwenyewe tafuta washauri wa kukusaidia. Hapa dar mtafute profesa Masalakulangwa yuko chuo cha tiba Kairuki- ni medical psychologist/mchungaji. Au mtafute mchungaji Hiza yuko Udsm chaplaincy. Hawa ni professional marriage counsellors na wazoefu. Hata kama we ni muislamu haisumbui ilimradi uwaambie kabla ili wajue wanatatua tatizo kwa mrengo upi. Yupo pia aunt sadaka lakini simfagilii kivile.
 
MKUU hapa mm sikuungi mkono hata kidogo na huyo mkeo sio chizi anasababu na haki yakufanya hivyo.

MKUU utakataa ilakiukweli kunasiku ulushawahi kulitibua kama miaka yote hiyo 8 umeishi nae vizuri na ukiwa na sim na hakuwa na tabia hiyo Leo hii ndio kaanza vibweka hivyo nakataa.

kama unampenda nakujiamini kweli na kama huna mchepuko sim ikipigwa ww mwachie apokee aongee nae au ikiwezekana unapopokea sim weka round speaker naye pia asikie ili roho yake ilizike.

lkn kama sim inapigwa mlikuwa mnaongea vizuri Mara una change unapokea sim nakutoka NJE kwanini asiwe na wasiwasi na wewe?.

MKUU kuwa mwazi kwamkeo bana na kaazungumza nae mbona mambo madogo sana haya.
 
Lakini huoni Kama ni kuonyesha kutoaminiana Kwa kiwango kikubwa tens unaonyesha mbele za watu. Kuna usemi Kuwa ukiona mtu hakuamini ujue na yeye si mwaminifu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom