OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT- Wazalendo imemteua Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Zanzibar) Juma Saanani kuwa Katibu Mkuu, Saanani anashika nafasi iliyoachwa na Samson Mwigamba huku Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama hicho ikitumia Ibara ya 29 (25iv) ya Katiba ya chama hicho kumteua Mwigamba kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama.
Uamuzi huo ulioridhiwa na Kamati Kuu (CC) umekuja baada ya siku tano ambapo Mwigamba alitangaza kung’oka Ukatibu Mkuu kwa kile alichokiita kwenda masomoni.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho inaeleza “uteuzi wa Mwigamba umefanyika kwa kuzingatia kuwa, Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi Makao Makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo”.