Mrisho Gambo, Tamaa ilimponza fisi

Mrisho Gambo, Tamaa ilimponza fisi

MAKOLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
618
Reaction score
280
gambo Korogwe.png

Ilikuwepo hadithi moja ya fisi iliyozua kisa cha "Tamaa ilimponza fisi" Mnyama huyu alialikwa kwenye sherehe mbili tofauti na zote zilifanyika kwa wakati mmoja. Fisi hakuwahi kuwa na busara na alipokuta chakula katika sherehe ya mwanzo hakijawa tayari alikwenda kwenye sherehe nyingine ili kuwahi makulaji.

Alifika na kukuta watu wanasafisha majamvi kuashiria kwamba tayari kumeliwa na akaamua kurudi sherehe ile ya awali ambapo napo alikuta tayari watu wameshakula"

Paliondokea bwana mmoja kwa jina la Mrisho Gambo aliyekuwa na majigambo kwenye zama za utawala wake.
Ikumbukwe kwamba Mrisho Gambo aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe aliyekuwa na mbwembwe na tambo nyingi za kiuongozi.

Ikumbukwe pia kwa sasa bwana Mrisho Gambo anasubiri huruma ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili apangiwe kazi nyingine baada ya uteuzi wake kutenguliwa hivi karibuni.

Leo katika ukurasa wake wa facebook ametokelezea akiueleza umma kwamba ametumiwa salamu nyingi na wana wa Korogwe ambao "eti" wanamsihi arudi na kuokota fomu ya ubunge katika moja ya majimbo mawili ya mjini hapo......

Hili halishangazi sana kwani ni haki yake, ila tayarai bwana Gambo alishawahi kujigamba kwamba anakwenda Ilala kuwakilisha wana Ilala huko Dodoma akiwa na lengo la kumpokea kijiti Mbunge wa sasa!

Ushauri wangu ni kwamba bwana mkubwa awe na msimamo kwani tamaa ilimponza fisi?
 
hawa wapambe wa riziwani wameshiriki vyema kuichafua serikali na ikulu kwa tabia zao.
 
Huyu jamaa hata mimi nilimshangaa sana nilipoiona ile post yake fb. Jamaa inaonekana hajajipanga kabisa. Sasa hivi kampeni zimeshaanza, yeye bado anatafuta jimbo la kugombea. Na kwa upande mwingine anaonekana kama vile haijui siasa (sorry for saying this). Kawaida kwenye siasa kuna watu wanaokuonea aibu, hata kama maji yapo shingoni, wao wataendelea kukupa moyo hadi pale hatua ya mwisho unapoteketea kabisa. Sijui ''sampling'' yake ya ''watu wa Korogwe'' kama anavyoiita mwenyewe kaichukuliaje, maana isiwe kukutana na wazee watano tu wenye njaa zao toka korogwe akajua ndio ujumbe wa wilaya nzima. Au Mkuu Gambo survey yako ni ile kupitia ''facebook wall'' yako? Kama ni ile, umepotea. Maana hata mimi pale niliku support tu kuwa uje Korogwe maana unanijua kwa jina, nikakuonea aibu, in reality, Korogwe ina wenyewe. Tafuta chaka mapema
Kwanza hana busara ya uongozi...!, yapo mengi tu ngoja niishie hapa
 
hawa wapambe wa riziwani wameshiriki vyema kuichafua serikali na ikulu kwa tabia zao.

Hayo yote ni matatizo yanayotokana na kuchagua viongozi wasiojua GOVERNANCE, kwasababu kama URAIS ni taasisi hutegemei kuwa mke wa RAIS au mtoto wake ashiriki katika kuteua watendaji wa serikali!!! The presidency is a noble institution that is protected by the constitution and not a collection of brainless family members.!
 
Haya ndio niliyoandika kuhusu Gambo few days ago

Wakulu Salaam,

Niliwahi kuandika hapa huko siku za nyuma kuwa Mrisho Gambo political career will be short lived. Nilitaja sababu zifuatazo

Bwana mdogo hayuko strategic kama kina Makamba. Ana pupa na papara. Ana mori na muku. Uongozi hautaki hivyo. Uongozi unataka plans, calculations and strategies.

Sababu ya pili ni kuwa bwana mdogo is poor in human resource management. Akifika mahali lazima awagawanye watu na kuwa na makundi ya wao na sisi.

Unlike viongozi kama kina Mandela ambao wanaleta unity where there is none and peace and justice where there is none. Gambo analeta makundi, vurugu na fujo mahala pa kazi.

Alipofika Korogwe kuna watu waliniambia kuwa Wakuu wa wilaya (kama Mawaziri) huwa wanakuja na kuondoka lakini sisi watendaji huwa tuko hapa daima (kama makatibu wakuu). Gambo amekuja na ataondoka atatuacha hapa.

Sababu ya Tatu Gambo alishindwa kuelewa kuwa Mkuu wa Wilaya ni mtu wa serikali kuu ( technicaly ni kama civil servant) na kuwa Wakuu wa wilaya sio Politician.

Gambo alikuwa anafanya kazi kama politician. Anataka umaarufu na mashindano. Anataka awe kwenye media kila mwezi. Anakodi waendesha pikipiki wampokee kwenye maandamano. Ukuu wa wilaya hautaki hivyo bwana mdogo.

Kaa kimya piga kazi utakuwa rewarded kama walivyofanya akina Mwongela na Dr Msengi.

Sababu ya nne ni unneccesary petty fights and drama - kutukana viongozi wenzako kuwa wana degree za chupi nk. Gambo alikuwa na viugomvi kila wakati vingi vikiwa visivyo na maana.

Sasa unapoanzisha maugomvi daily huwezi jua - kuna siku utakwaa visiki. Uongozi hautaki hivyo. Katika Kitabu Chake cha the Art of War Sun Tzu aliandika kuwa "you must know how to choose your battles" sio kila vita ni lazima upigane zingine unaacha zipite.

Sababu ya tano ni kuwa Gambo yuko kwenye kundi la LARGER THAN LIFE CELEBRITY LEADERS kama Trump. Hawa huwa sio sustained leaders. Huwa wanakuja na kupita kama kimbunga

Kwakifupi uongozi wa Gambo ni uongozi aliopata kwa bahati mbaya kwakuwa serikali ya awamu ya nne ni serikali ya wajanja na makanjanja kama Makonda na Nyalandu.

Watu kama hawa wasingekuwa na nafasi kwenye serikali makini kama ya Nyerere au Mkapa. Na watu hawa wataondoka punde makanjanja watakapomaliza awamu yao ya nne awamu ya akina kawambwa, hawa ghasia, lazaro nyalandu, nk

Nchi yetu inapita katika kipindi cha mpito. Lets hold on tight, kipindi hiki kitapita nasi tutarudi kuendelea kujenga nchi yetu. Awamu ya nne ni THE LOST TEN YEARS
 
Huyu jamaa hata mimi nilimshangaa sana nilipoiona ile post yake fb. Jamaa inaonekana hajajipanga kabisa. Sasa hivi kampeni zimeshaanza, yeye bado anatafuta jimbo la kugombea. Na kwa upande mwingine anaonekana kama vile haijui siasa (sorry for saying this). Kawaida kwenye siasa kuna watu wanaokuonea aibu, hata kama maji yapo shingoni, wao wataendelea kukupa moyo hadi pale hatua ya mwisho unapoteketea kabisa. Sijui ''sampling'' yake ya ''watu wa Korogwe'' kama anavyoiita mwenyewe kaichukuliaje, maana isiwe kukutana na wazee watano tu wenye njaa zao toka korogwe akajua ndio ujumbe wa wilaya nzima. Au Mkuu Gambo survey yako ni ile kupitia ''facebook wall'' yako? Kama ni ile, umepotea. Maana hata mimi pale niliku support tu kuwa uje Korogwe maana unanijua kwa jina, nikakuonea aibu, in reality, Korogwe ina wenyewe. Tafuta chaka mapema
Kwanza hana busara ya uongozi...!, yapo mengi tu ngoja niishie hapa
Mkuu, huoni kuwa nawe umechangia kumpotosha kupitia ukurasa wake wa facebook sababu umesema ulimsapoti fb huku ukijua kabisa kuwa hawezi kushinda Korogwe. Ingekuwa vizuri ungemweleza wazi akakaa anajua kuliko ulivyofanya fb.
 
Back
Top Bottom