Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,390
- 4,090
Siungi mkono wavuta bangi wa mitaani wanaoona ujanja kuvuta na kutumia herb vibaya, naunga mkono medical marijuana na spiritual. Ambao wanaotumia kwa ustaarabu na wasiowakera watu.
Maelezo yako yanashawishi sana. Tatizo liko hapo kwenye nyekundu. Hao unaowasema wanaitumia vibaya ndio wanaoonekana zaidi hadharani. Yaani wamekuwa ndiyo "public face" ya watumiaji wa bangi. Kama ilivyo kwa wanaotetea pombe kwamba inaweza kunywewa "kistaarabu" bila kuleta madhara wala kero kwa jamii, itakuwa vyema pia ukitoa elimu kuhusu udhibiti unaopaswa kuchukuliwa ili bangi ikiruhusiwa basi wasiwepo hao "watumiaji wabaya". Na maelezo yako yazingatie mazingira halisi ya utawala wa nchi yetu uliosongwa na uroho mkubwa wa pesa (excessive greed), rushwa, uzembe, kutojali, n.k. Nasema haya, ili kuhakikisha kama wazo lako linawezekana (feasible) hapa Tanzania ili tusijekuta pamoja na matatizo (wanaita changamoto) kibao tuliyonayo, tunaishia pia kuelemewa na machizi walio-abuse hemp.