Pole sana,
1: Temeke RRH, hawana MRI bali wana CT scan. Ila suala la msingi ni kujua ni kipimo kipi kinahitajika kulingana na tatizo la mgonjwa.
2: Unaweza kuomba referral kwenda Muhimbili, ni kujenga hoja tu.
3: Ni vyema pia kuwasiliana vyema na daktari anaemhudumia mgonjwa ili kujua/kuelewa zaidi:
A: Tatizo la msingi la mgonjwa kulingana na malalamiko mengine.
B: Mtizamo wa vipimo zaidi kwa mgonjwa.
B: Mwendelezo wa tiba ya mgonjwa husika.