Mrembo ndotoni

Mrembo ndotoni

Rauyah

Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
28
Reaction score
13
Wanajamii nawasalimu.

Kila mtu huwa na Ndoto na njozi.Kwa Muda wa wiki mbili sasa
nimekuwa nikiota ndoto ya ajabu.Ndani ya ndoto hiyo namuona binti mrembo akiwa amesimama kando ya bahari huku gauni lake la samawati likipeperushwa na upepo mwanana wa bahari.Sura yake ni ya mviringo na yakuvutia.Macho yake yanaita vilivyo.Vidani vyake vinawaka mithili ya nyota.Hereni masikioni,mkufu shingoni,bangili mikononi na vikuku miguuni.Mara nyingi namuota akiwa anacheza taratibu na kwa mahaba.Mara nyingine huwa amesimama tu akiangalia baharini huku upepo ukipuliza nywele zake za singa.Kila napojaribu kumgusa ndo huwa nashtuka nakujikuta niko mwenyewe kitandani.Sura yake sijawahi kuiona sehemu nyingine zaidi ya kwenye hiyo ndoto.Kinachonishangaza ni kwamba ndoto hii hujirudia mara kwa mara.

Jamani naomba wenyekujua kutabiri ndoto wanidadavulie maana naanza kupata woga.Au ndo jini mahaba huyu?
 
Uyo ni jini mahaba hapo hakuna cha kuuliza CHA KUFANYA UWE UNASALI NA KUSEMA NAJIFUNIKA KWA DAMU YA YESU NA ITAKUA VEMA UKIWA UNASOMA BIBLE KABLA HUJALALA,NI HATARI SANA KUENDEKEZA HLO UTAPATA BALAA NA MIKOSI.
 
Uyo ni jini mahaba hapo hakuna cha kuuliza CHA KUFANYA UWE UNASALI NA KUSEMA NAJIFUNIKA KWA DAMU YA YESU NA ITAKUA VEMA UKIWA UNASOMA BIBLE KABLA HUJALALA,NI HATARI SANA KUENDEKEZA HLO UTAPATA BALAA NA MIKOSI.

ndgu funguka vyema wote tujue.. Balaa na Mikosi kivipi?
 
enjoy ndoto yako na usahau maana yake kwani jina lako 'Rauyah" pia maana yake ni ndoto
 
Daaahh!! Pole sana ila la msingi km unamwamini mungu omba tu mzee!! Km ni mazuri yanatokea yatimie kama ni mabaya ayaepushie mbali!!
 
Hhahahahah lol imenikumbusha movie ya ki ghana nimetizama juzi jina CHELSEA may be she's ur true if she exist

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom