Pole sana Mkuu kwa kumpoteza mwanao kwa mazingira yanavyoonesha.
Kwa nini baadhi ya wadada wana roho katili kiasi hicho lakini? Bahati mbaya wanatafsiri mtu ni aliyezaliwa tu. Wamepotoka akili na ufahamu wao. Mtu ni Nafsi na sio mwili, Mimba ikishatungwa tayari ni Mtu hai awe na wiki mbili au miaka 100 tofauti yao ni maumbile tu na akili, ila ana nafsi hai kabisa. Huo ni uuaji mbaya zaidi kuwahi fanywa na mwanadamu aliye na akili na ufahamu.
Kweli inaingia akilini kuua mwenzako(mimba) ili jamii ikuone decent? Kwani hiyo jamii ni safi kiasi gani bandugu? mbona hao mnaotaka wawaone decent nao ni wachafu kuliko wewe?? endeleeni tu kutoa, lakini ipo siku mtatoa hesabu ya hao watu/nafsi hai mlizoua. a
Hivi ingekuwaje mama yako angefanya hivyo, sio ndio wewe ungekufa? then mbona mwasema mimba changa sio mtu kamili? Kwani hiyo nafsi yako ambayo ndio wewe ilikuingia baada ya kuzaliwa? kwani kuua si kutenganisha mwili na nafsi??? Tafadhalini sana dada zetu, Hakuna uasi mkubwa kwa Mungu kama kutoa Mimba!!