Mrembo gani katika hawa alitupatia ngoma kali zaidi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
MREMBO GANI AMETUPATIA NGOMA KALI ZAIDI????
Orodha hii inakuletea warembo watano waliosumbua akili za wasanii wa Bongo fleva mpaka wakawaandikia nyimbo.

1. CHRISTINA MANONGI "SINTA"
Juma Nature alizama hapa na kutengeneza celebrity couple ya awali kabisa na pengine bora zaidi kwenye kiwanda hiki.

Mambo yalipoenda arijojo, Nature akammaliza Sinta kwa SITAKI DEMU na INANIUMA SANA, ambamo alimtaja mpaka jina na wasifu wake (umaarufu, uanafunzi wa DSJ na uzuri wa sura)

Kuna nyepesi niliwahi kuzipata kuwa hata Cool James mwana wa Dandu alipoandika remix ya SINA MAKOSA alimlenga Sinta (japo sikupata UHAKIKA wa hili)

Kwani Sinta aliishia hapo? Aliimbiwa na JUMA Nature, miaka kadhaa baadaye akashirikishwa kwenye video ya JUMA mwingine, round hii alikuwa JUMA Kakere, kwenye video ya POLE KWA SAFARI. ITAFUTE MTANDAONI ile video halafu Sinta alivyokuwa "mali" sasa!!

Mr Paul kwenye ngoma yake ya PENZI KITI CHA BASI, anasema penzi likiisha WANAZUSHA ANA NGOMA, TENA MBAYA MBAYAAAA! Binafsi naona Paul alimchimba Nature na kumtetea Sinta kuwa hakuwa na ngoma ila Nature aliyasema yale KUTOKANA na HASIRA.

Joh Makini kwenye ULIMWENGU WA WAPENDANAO anasema: "LEO SITAKI DEMU, KESHO I NEED YOU MAA! KESHO KUTWA AH! WAPI ZILIKUWA TU NI TAMAA"

Kwa ambaye umeachwa hapa, iko hivi; Nature alimchana Sinta kwenye SITAKI DEMU halafu alipotoa album ya UBINADAMU KAZI, kuna ngoma moja kalia sana humo anasema RUDI NYUMBANI MAMA! halafu miaka kadhaa baadaye, Nature AKATOA ngoma inaitwa AH WAPI!!! Humo ndani anaonesha kuwa aliachana na mpenzi wake sababu ya WALIMWENGU!!!

Umeelewa namna Joh alivyommaliza Nature na kusimama na Sinta??
Je ni ngoma ngapi Zina uhusiano wa moja kwa moja na Sinta mbali na hizi???
1685259108274.jpeg


2. NANCY SUMARI
Eee bwana eeeh! Mbwana Ally Mohammed kutoka Manza Bay, Mabibo/ Makuburi mpaka MANZESE kwa Bonge na Tale "alijaza" ngoma kuhusu Nancy Sumari, miss Tanzania mwaka 2005 kwenye album yake.
INA MAANA ni ngoma ambayo Mb Doggy alimtaja Nancy kwa jina kabisa. Ukisikiliza MAPENZI KITU GANI, japo kataja vituo vya redio lakini bado unaona Doggy analia na ambaye anamuuliza INA MAANA hajui kama anampenda!! Humu anasema unayempenda yeye hakupendi.

"UZURI WA SURA YAKO UMEKUFANYA WAKUPE TAJI LA AFRIKA" Baada ya kushinda Miss Tanzania, miezi kadhaa baadaye, Nancy AKASHINDA taji la Miss World, Africa.

Wapo waliosema Doggy alimpenda sana Nancy (kuliko mimi mwandishi wenu) huku wengine wakisema Doggy alitumika kufikisha hisia za Bonge kwa Nancy (nilikuwa skuli kwa kipindi hicho, sina hakika na ukweli wa fununu hizi)
1685259079904.jpeg


3. WEMA SEPETU
Miss Tanzania 2006 huyu mbele ya Jokate Mwegelo (niliyemkubali sana kwa kipindi kile)
Umaarufu wake ukiwa kwenye kimo cha chini kabisa, Herry Sameer "Mr Blue" alikuwa anajifaidia mema ya nchi.

Mara huku na kule, Khalid Mohamed "TID" akatia unyama mwingi, Wema akahama timu kutoka "team Mapozi/Micharazo" mpaka upande wa "Top band"

Tid alivyo "mbaya" akamchek Blue aingize voko kwenye NILIKATAA na kumchana Wema kuwa ni kicheche, Tid hakuishia hapo, akamwita Chila na Dully na kuangusha dude; KAMA UNAKUJA BABY NJOO, KAMA UNAKWENDA BABY NENDAAAA, SIWEZI KUSHEA MAPENZI NA WALE SABABU MI NI BONGE LA STAAAA, KAMA HUJANIONA KWENYE TV UTANSKIA KWENYE REDIOOOO

NAWABURUZABURUZA WAKO MABISHOO OOOOO OOOOH! Humo Wema alipakwa sana
Blue akaona haiwezekani, akaenda kwa "mchawi" wake, Roy Bukuku na kuangusha ROHO ZAWAUMA na humo akamtaja mpaka jina; NAKUPENDA WEMA SITOMPENDA MWINGINE ( NIELEWE) CHAGUO NI WEMA, SITOMPENDA MWINGINE (NI WEWE)

Byser sasa alivyo mtoto wa mjini, alipoulizwa, akasema alimaanisha "NAKUPENDA WE- MA" IKIWA KIFUPI CHA "WEWE MAMA" na siyo Wema tuliyemfahamu sisi.

2009/2010 Nassib Abdul akawa Diamond Platnumz, staa gani huna mali Kali?? Naye akanasa kwa Wema na kutuletea ngoma kama; NASEMA NAWE, SIKOMI ambazo zilikuwa na lengo la kumkejeli Wema (Nikumbusheni nyimbo ambazo Diamond alimsifia Wema)
1685259059450.jpeg


4. KAJALA FRIDA MASANJA
Kuanzia dances zake kwenye majukwaa, mpaka kuishi na kuwapokea wasanii walioenda Bamaga pale kama P hakuwepo mpaka kuishi kinyumba kabisa na P FUNK MAJANI na kumzaa PAULA mpaka kuzinguana na kumfanya Majani ajipe likizo ya muziki ili asahau jana yake na Kajala.

P akavumilia na kushindwa, akarudi studio kwa lazima na kumwita Dully, wakatoa PLEASE FORGIVE ME, Majani alielezea hisia zake zote humu.

Akaona haitoshi, akatengeneza beat nyingine ambayo alitaka aombe msamaha kwa Kajala kwa mara nyingine lakini Madee akaingia studio na kuikuta beat Ile iliyokuwa na hook kabisa, Madee akavaa hisia za Majani na kuandika mistari mikali mno, goma likatoka, YOTE MAISHA. Majani kaua sana kuanzia intro, chorus mpaka outro.

Ni sahihi tukisema Kajala "katuulia" Bongo Records lakini alitupa ngoma kali mbili.
Kizazi kikapita, kikaja kipya, bwana Rajab akapandisha hadhi ya jina lake na kuwa Harmonize, akatuletea ngoma kama; VIBAYA, KAMA UNAMJUA, DEKA, NITAUBEBA mpaka SINGLE AGAIN. Zote hizi mada yake kuu ni Kajala. Ukimchek huyo Kajala mwenyewe, huwezi kumcheka wala kumshangaa Mmakonde.
Usisahau pia Kajala ndiye Yule mrembo anayemtoa nishai Prof Jay kwenye video ya ZALI LA MENTALI kwa kumwona Jay hana ishu.
1685259035150.jpeg

5. NAJMA "NAJ"
Hii chombo ya "Kihindi" aseee ni noma. Nilikuwa na gazeti la BAABKUBWA ambapo ukurasa wa katikati ulikuwa na picha za Mr Blue na Naj, kila nikitoka skuli nilikuwa nazikodolea.

Si UNAIKUMBUKA TABASAMU??? basi Yule video queen ndiye Naj MWENYEWE. "BLUE VIPI MBONA SIKUSIKII TENA? SIKUSIKII UKIFLOW, MBONA SIKUSIKII UKISEMA? NIKO BIZY NA BABY JAMANI NSHASEMA, NIKO BIZY NA WIFE JAMANI NISHASEMA"

Hata ningekuwa mimi, ningekuwa bizy kama Babylon ningepata toto kama Najma.
Miaka kadhaa baadaye "super black" Baraka kutoka Mwanza kwa Kid Bwoy akatua jijini na kujibebea mzigo na kutengeneza BANA (BARAKA na NAJMA)
1685259127639.jpeg

Sina KUMBUKUMBU za Kama BARAKAH ana nyimbo alizoandika kuhusu Naj iwe kwa kumsifia au kwa kumponda!! Kama zipo, Nikumbusheni.
Nani kasahaulika kwenye orodha?
Ngoma gani zinawahusu na nimezisahau??
Mrembo yupi unaona kabisa ALISTAHILI kuandikiwa hata albums tatu?
LUAH
270523
 
Sahihisho:
"Ah wapi" ni kutoka album ya ugali iliyoitangulia album ya "Ubinadam kazi" yenye Rudi nyumbani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom