Mrema: Polisi wanasambaza dawa za kulevya

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,404
24,990
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.
mremahuyo.jpg

Augustino Mrema - Mwenyekiti Bodi ya Parole

Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.

"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema

Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.

"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.

Chanzo: IPP Media
 
Haya mapyaaaa. Hivi kumbe huyu mzee hajafa bado....

Tangu alivyosema boda boda wakaripoti kwake wakisumbuliwa ba polisi basi namuonaga mpuuz tu
 
Vita ngumu duniani ni
1. Madawa ya Kulevya
2. Rushwa na Ufisadi
kwa sababu wanaohusika moja kwa moja pia wanaoshirikiana wa wauzaji ni

1. Wanasiasa wakubwa/maarufu / wabunge pande zote watawala na wapinzani
2. Viongozi/wafanyakazi mbalimbali ndani ya serikali
3. Mahakama
4. Polisi kwa ujumla
5. Baadhi ya wanajeshi na maofisa wa usalama
6. Waendesha Mashtaka

Wote hao ndiyo unategemea waendeshe hiyo vita dhidi ya madawa ya kulevya na rushwa na ufisadi LAKINI kwa kuwa wao wanufaika, si rahisi kuvitokomeza. Kila atakae anzisha maana yake ataanza kushambuliwa kila kona kwa naona tofauti huku vyombo vya habari vikikoleza kwa kupewa pesa au nao kuwa washiriki.
 
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.

c5be1e586025684f64625eafbd43b47a.jpg

Augustino Mrema - Mwenyekiti Bodi ya Parole

Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.

"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema

Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.

"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.
 
Kwa mwendo huu nadhani hili la madawa ya kulevya limekuja ili kufunika mambo kama njaa, matokeo mabovu ya ufaulu, hali mbaya ya uchumi na madudu yanayoendelea awamu hii. Halina mashiko wala nia ambayo baadhi ya watu wameshaamini kuwa ndio iliyokusudiwa.
 
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.
mremahuyo.jpg

Augustino Mrema - Mwenyekiti Bodi ya Parole

Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.

"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema

Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.

"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.

Chanzo: IPP Media
Macho huwa yanaona na Moyo unaongea letu jicho
 
Sijuhi watu wanawaza nini tu..
Yaani ushinde vita vya madawa ya kulevywa kirahisi rahisi tu hivi?
Ukahaba, ujangili, rushwa, uchawi, ushirikina na madawa ya kulevywa ni miongoni mwa very old professions. Ni hulka za binadamu hizo!
Muhimu ni kutumia hizo fursa kuwapa watu ajira zilizo rasmi na kuongeza mzunguko wa pesa mtaani.
Mfano kwa kutunga sheria kali kali, kuunda tume imara, zenye meno na bajeti ya kuajiri na kukidhi mahitaji ya utendaji n.k.
Badala ya kuwaza kutokomeza yasiyowezekana ni muhimu tuwaze kubuni fursa za kukuza uchumi
 
Vita ngumu duniani ni
1. Madawa ya Kulevya
2. Rushwa na Ufisadi
kwa sababu wanaohusika moja kwa moja pia wanaoshirikiana wa wauzaji ni

1. Wanasiasa wakubwa/maarufu / wabunge pande zote watawala na wapinzani
2. Viongozi/wafanyakazi mbalimbali ndani ya serikali
3. Mahakama
4. Polisi kwa ujumla
5. Baadhi ya wanajeshi na maofisa wa usalama
6. Waendesha Mashtaka

Wote hao ndiyo unategemea waendeshe hiyo vita dhidi ya madawa ya kulevya na rushwa na ufisadi LAKINI kwa kuwa wao wanufaika, si rahisi kuvitokomeza. Kila atakae anzisha maana yake ataanza kushambuliwa kila kona kwa naona tofauti huku vyombo vya habari vikikoleza kwa kupewa pesa au nao kuwa washiriki.
Haya ni mapambano ya magenge ya wafanyabiashara hii haramu. Mapambano Kati ya wauzaji walio madarakani na waliowaweka madarakani. Tusubiri
 
Back
Top Bottom