Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwenye viwanja vya Fire mjini humo, wakati wa mkutano kujadili amani na kuienzi ulioandaliwa na uongozi wa taasisi ya Alshabab Islamic Daawah ya Morogoro. (Picha na John Nditi).
hivi kumbe hata TZ alshabab wapo?
naomba anayejua maana ya "alshabab" atueleze ili kututuliza roho, mwenzenu hata kusikia tu hili neno nasikia nyele zikisimama kichwani!
source: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
Shabab maana yake ni kijana.Hivyo hiki ni kikundi cha vijana(youths) ambacho kinakusudia kuwazindua waislam hasa vijana kwa kuwa wao ndio taifa lenye nguvu na muono wa maendeleo kiuchumi na kiimani.
linaandikwa hivi Al-shabab
katika kiarabu Al=The na Shabab=Youth(kiswahili tuseme Vijana,kwani umoja wa neno Shabab ni neno Shab na wingi wake ni Shabab)
kwahiyo usiogope lugha wala haina maana mbaya, kwani hata wewe ni shab na ukiwa na vijana wenzako nyinyi ni mashabab.
Al-shabab Islamic Dawah=The Youth Islamic Dawah.
Ni kama alikuwepo sinza akisali jpili ya leo....huyu mheshimiwa nikimuona tu huwa najisikia furaha isiyo na kifani maana ndio mtu wa kwanza kumuona anavaa nguo kama graduate baada ya kupata degree confirmation kwa fax....I want to use his tricks to get Masters and PHd halafu nikodi gari ya wazi nikiuthibitishia umma kwamba ni kweli nimepata elim hiyo....kila mtu ana role model wake na kwasababu fulani, lol!