Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
AGUSTINO Lyatonga Mrema (TLP), aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo (2010-2015) amefuta kesi ya kupinga ushindi wa James Mbatia (NCCR-Mageuzi) kwenye jimbo hilo.
Kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana, pande zote mbili zilikubaliana kuondoa kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi.
Kesi hiyo imeondolewa mahakamani baada ya January Nkobogho, Wakili wa Agustino Mrema (TLP) kuwasilisha ombi la mlalamikaji mbele ya Lugalo Mwandambo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi aondoe kesi hiyo kutokana na kuwapo maslahi mapana ya umma.
Wakili Nkobogho amesema, kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi kwa wapiga kura wa Jimbo la Vunjo pamoja na kupunguza gharama kwa serikali ya kuendesha kesi hiyo mlalamikaji na mlalamikiwa wameridhiana kuondoa kesi hiyo mahakamani.
Mbatia ameliambia gazeti hili kwamba, ‘nilimshauri Mrema agombe udiwani nitamuunga mkono.”
Amesema “Ningemuunga mkono, chama changu kisingeweka mgombea kwenye kata ambayo amegombea na tungemsaidia kampeni ashinde lakini Mrema alikataa.”
Kauli ya Mbtia kumtaka Mrema agombee udiwani badala ya ubunge ilikuwa ni fedheha kubwa kwa mtu ambaye alitikisha nchi katika siasa za vyama vingi 1995.
Mrema alikuwa mtu wa pili nyuma ya Benjamin Mkapa aliyekuwa mgombea wa urais CCM mwaka 1995 ambapo alipata asilima 31 ya kura.
Wakizungumza nje ya mahakama baadhi ya mawakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendela na Youngsaviour Msuya wamempongeza Mrema kwa uamuzi wake wa kuridhia kumalizika kwa kesi hiyo.
Mbatia ameahidi kuendelea na ushirikiano na Mrema kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Vunjo na kuahidi kulipa asilimia 50 ya gharama za mawakili.
Source: Mwanahalisi