Mrema 1995 na Lowassa 2015

Mrema 1995 na Lowassa 2015

Freedom tommorrow

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2015
Posts
1,795
Reaction score
1,132
Itakumbukwa kuwa ndugu Augustino L. Mrema alijaribu bahati yake ya kukiwania kiti cha urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995 kupitia NCCR mageuzi lakini alishindwa. Kulikuwa na sababu za kushindwa katika miaka ile. Sababu kubwa za msingi ni 5.

1. Uwepo wa baba wa taifa: Kipindi kile nyerere alijitahidi sana kuhakikisha kuwa chama cha CCMwanabaki kuwa wamoja na mrema anakosa uraisi. Hivyo alitembea sehemu kubwa ya nchi na kuhakikisha kuwa watu wanamkubali mkapa na wanachagua CCM. Kukosekana kwa mshikamano ndani CCM na kutokuwepo kwa baba wa taifa ni advantage kubwa kwa lowassa

2. Vijana wengi kutojiandikisha kupiga kura: Mwaka 1995 vijana wengi walijitokeza kuwa washabiki wa mrema lakini ukweli ni kuwa wengi walikuwa hawakujiandikisha kupiga kura. Hivyo mrema alijikuta akipoteza nafasi hiyo kirahisi dhidi ya mkapa.hali hiyo ni tofauti na 2025 kwani sensa inaonyesha vijana ni 52% na wengi wamejiandikisha hiii itampa advantage lowassa

3. Kampeni za CCM kuwa wapinzani wanaleta vita: CCM walikuwa wanatumia mikanda ya video ya nchi yenye vita ili kuwatisha wananchi wasiwachague wapinzani, na kweli watu wengi waliamini hivyo hilo kwa sasa halipo tena. Kuelewa kwa wananchi maana ya kuwepo upinzani na faida zake kwa sasa ni advantage kwa Lowassa

4. Msiba wa John Komba: hii pia ni advantage kwa lowassa kwani yule bwana alikuwa na kipaji kikubwa sana cha kuwavutia watu hasa kina mama kwa muziki wake mahili jukwaani.

5. Wananchi kutoelewa maana ya upinzani: CCM walieneza kasumba mbaya sana kama wapinzani ni watu hatari, hii iliifanya mpaka siasa ya zanzibar zikawa za chuki na huku bara watu waliogopa upinzani kwa sasa ni tofauti kabisa, hii ni advantage kwa Lowassa

Hitimisho: CCM inaondoka
 
Tutaungana Arusha Moshi na mikoa mingine kumpeleka Lowassa Ikulu kwa namna yeyote ile. Wao waandae mabomu na marisasi yao.
 
Ghana,Zambia,Germany na sehemu nyingine za dunia Haya yametokea.Mtu anatoswa huku na kupokelewa kule afu anashinda
 
Wapinzani kumwita el fisadi na leo kusimasha urais itawasumbua blue haiwezi kuwa nyepe
 
Ghana,Zambia,Germany na sehemu nyingine za dunia Haya yametokea.Mtu anatoswa huku na kupokelewa kule afu anashinda

Ebu tudadavulie kidogo mifano yako, yaani tuambie kule Zambia ni mwanasiasa yupi alitemwa na chama tawala na kuingia ikulu kwa tiketi ya upinzani, vilevile Ghana na ujerumani yalitokea hayo mwaka gani, chama gani, marais gani ?
 
Kwanza kumfananisha mrema na lowassa ni kosa kubwa! Pili ndani ya miaka 20 mambo mengi yamebadilika. Kikwete ameisha sema mara nyingi, ccm wajiandae kisaikolojia, ccm inawezekana kushindwa uchaguzi 2015. Yametimia
 
Wakubwa wa CCM hawakupenda kuona chaguo la walio wengi, masikio walitia pamba kali, machoni wakavaa miwani za mbao, hata walipojaribu kutekenywa na wanec walioimba TUNAIMANI NA LOWASSA hawakupenda kujali.
Nyerere aliwaambia...msipuuze maoni ya wananchi walio wengi. Channel ten hawakuchoka kuwakumbushia ujumbe huu mara kwa mara.... haikusaidia.
Kuna jinsi moja tu ya kuwafikishia ujumbe watu wsio penda kusikia. SANDUKU LA KURA.
1995 watu walikua hawajaichoka CCM ki vile . Mrema angeungana na wenzie angechukua nchi. Leo hii ni kiongozi gani wa CCM unadhani anaweza akawakusanya wananchi na kuwakonvinc kama Nyerere 1995,
watayaoga
 
Ingawa kuna vitu vinaeleweka kwenye huu uzi wako lakini mpangilio wako wa kuleta hoja haukuwa mzuri.
Ni sawa CCM INAONDOKA MADARAKANI.
 
Mrema hakuwa na Fedha wala mikakati ya Ushindi, yeye alitarajia apewe ushindi kwa kuwa tu atapata kura Nyingi, safari hii ukishinda kwa bao la Mkono refa anaporwa filimbi kabla hajapuliza kuashiria goli. Cha msingi tuombee Amani nchi yetu
 
Low thinking ya huyu mkwere anayeishi pale magogono ndio inaipeleka CCM shimoni. Honestly jamaa hana vission...,
 
Ningekuwa JMK mara tu baada ya mkutano wa Dodoma, ningeitisha mkutano mkuu wa chama kuvunja makundi na kila mtu aliyekatwa kwa haki au hila apewe nafasi ya kuongea na kueleza ya moyoni. Lakini ....
 
Huu uchaguzi utakua mtamu sanaaa.

Mamvi anaweza akachukua mjue.
 
magufuli atapata kura 50% kanda ya ziwa na dodoma tu kwengine 0%.

Kanda ya ziwa ya wapi? Labda geita tu na sengerema, possibly na Tabora😯 kule mara , kagera, mwanza mjini, bunda, atasubiri sana
 
11755858_10153475617134339_3098498111802194751_n.jpg
 
Miaka 20 ni mingi sana katika siasa, na mbinu za mrema na Edward ni tofauti kabisa,
Kumbuka kuwa hata jakaya bila Lowasa leo asingekuwa raisi.
 
Back
Top Bottom