Mrejesho tiba ya mkojo

Mrejesho tiba ya mkojo

SWEET RIZIKI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
288
Reaction score
387
Habari wana jamvi. Miezi kama Mitano hivi iliyopita kuna mwanajamvi aliweka thread hapa akieleza jinsi mkojo unavyoweza kutibu Jino na Vidonda vya Tumbo.

Binafsi nilikuwa nasumbuliwa sana na vidonda vya Tumbo hali iliyonitishia kufunga Mwezi Mtukufu. Nimezoea kufunga pia Suala jingine nililokuwa nafikiria ni ile Faini ya Kulisha Masikini kila Siku kwa Siku zote 30 za Mfungo wa Ramadhani kama sitoweza kufunga kutokana na Maradhi. Nilipiga hesabu kwa kima cha chini kabisa ni 7000 * 30 = 210,000/= . Bado nitoe Zakat Fitiri Kilo 3 za Mchele kwa kila mtoto na Wakishamaliza Kupendeza Sikukuu July Niwasafirishe kwenye kwenda Shule.

Nilisali na kuomba Mungu anisaidie niweze kupata dawa niendelee kufunga sababu pia nisingeeeza bila kufunga nishazoea ni Mila niliyokulia nayo. Baada ya kupitia thread mbalimbali ya dawa za Vidonda vya Tumbo humu JD nikakutana na Post ya Mkuu mmoja hivi nishasahau Id yake ikieleza dawa ya Mkojo wa Asubuhi Dozi ya Siku tatu mfululizo.

Ilibaki Siku kama Tano kuanza Mfungo wa Ramadhani 2017 na hali yangu ilikuwa dhaifu, basi nilijipa moyo nikaondoa kinyaa ambacho kimenijaa, nikaanza Siku ya Kwanza , ya Pili na ya Tatu. Baada ya hapo nikaona Tumbo kimya. Siku ya NNE nikakaa nusu Siku bila kula nikaona Tumbo kimya. Niashukuru Mungu , Siku ya Tano Kimya ya Sita Ramadhani nikanuia nikaanza mzigo ,

Wakuu Nawashuhudia Nilimaliza Mfungo na Sita nikafunga Siku NNE baadae nikaanza kusikia Vichomi Tumboni nikaacha nikatafuta Magnesium likapoa. Lakini tangu July hadi leo hata nikae hadi SAA Kumi Tumbo halinisumbui najiona Kama Nimepona Vidonda Vya Tumbo na Jino kwa Gharama Zero 0 kupitia Tiba ya Mkojo wangu mwenyewe.

Basi nitoe Wito tu kwa wale Wanaosumbuka na Vidonda vya Tumbo na Meno Vaaeni Ujasiri jitibu wenyewe , tuache kujinyanyapaa kwani hata hizo dawa za Viwandani au Za Waganga wa Asili hatujui wanaweka nini, Mimi nimepona sipendi nawe Uteseke.

Pia nimekuja ona Tiba nyingine tena ya Mkojo ni kama kuna MTU ameanguka vile kama degedege au kifafa watu huenda Msalani au bafuni zile za sakafu ya Asili na kuchukua ule udongo uliolowana na kumpaka. Mtu akinywa sumu au kazidiwa na pombe pia watu humnywesha Mkojo na anaamka.

Sijui kitaalam kuna nini kwenye Mkojo.

Karibu na Ahsante Jf Doctor be blessed. Amina.
 
Kuna wadada wanadanganyana ni limbwata. Jaribu na hili utuletee mrejesho
 
mkuu Nina shemeji yangu anasumbuliwa na vidonda vya tumbo, ningependa unifafanulie yaani unipe maelezo dawa inatumikaje, inaandaliwaje, doz kipimo chake. nitashukuru sana mkuu wangu cc. SWEET RIZIKI
 
Suala la. Mkojo kipindi nipo mdogo umri wa kati ya 8-10, enzi hizo tulikuwa tunasumbuliwa na maupele kwenye ngozi.

Mzee wetu alituambia tupake mkojo wa Ng'ombe ule wa Asubuhi.

Tulikinga mkojo na tulipaka tukafanikiwa kupona.

Kwa hakika mkojo ni dawa, wa ng'ombe ulitibu upele na sasa ndugu yetu kathibitisha mkojo wa binadamu kwenye tiba ya ulcers.
 
Magonjwa ya U.T.I kisonono Kaswende.Kichocho na mengine mengi yanatambulika kupitia kupima mkojo.ni kwa fikra zangu je VIP ukinywa mkojo na pengine upo ktk maambukizo ya magonjwa hayo bila kujua si ndo kupeleka bacteria tumbon tena au..
 
Aiseee! Hivi ile dawa walikua wanaita mkojo wa punda bado ipo?
 
mkuu Nina shemeji yangu anasumbuliwa na vidonda vya tumbo, ningependa unifafanulie yaani unipe maelezo dawa inatumikaje, inaandaliwaje, doz kipimo chake. nitashukuru sana mkuu wangu cc. SWEET RIZIKI
Yaani mkuu Dozi yake ni Siku Tatu mfululizo . Ni ule mkojo wa kwanza wa Asubuhi , kipimo kwa kweli haiwezi kuzidi kikombe kidogo maana ni Kali kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom