Mrejesho: Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

raphael linkala

New Member
Jan 4, 2016
2
27
Wadau nawasalimu,

Nashukuru kwa ushauri mlionipa jana kwenye habari hii yahttp://www.jamiiforums.com/threads/mke-wangu-hapendi-kuongozana-na-mimi-barabarani.994983/#post-15025211 kwa tatizo langu, wengi mliniuliza maswali sikuweza kujibu kwa sababu zilizokua nje ya uwezo, hata hivyo kwa mawazo yenu na ya kwangu mwenyewe nimepata ufumbuzi

Kuanzia sasa sitatoka outing yeyote ile na wife, nitatoka na mwanamke mwingine mwenye upendo na mm, ambae ni mdogo wake na wife, anajali, anajali na hajawahi kunikwepa, na nnahisi ananipenda kkwa dhati.

Kuna mliosema huenda wife ananizidi kipata, cheo, class etc, hii sio kweli, alipo graduate alinikuta tayari mm ni mwajiriwa wa NMB, nilipomuoa nikachakarika nae akaingia hapo, NMB nikaona si vizuri kufanya pamoja nikahamia bank nyingine kwa nafasi ya juu kuliko ile ya mwwnzo ingawa si kubwa sana, yeye akaendelea huko huko hadi sasa kama mfanyakazi wa kawaida, hivyo kwa maana ya career na maisha nipo juu yake, ingawa tunaendesha maisha pamoja kwa maana ya ushirikiano wa kiuchumi etc.

Pia mimi ni mtu naejipenda, naenda kwa fashion, manukato, wapo akina dada wanaenda uturuki wanatuletea nguo za kisasa na manukato pale ofisini, hata kama hatuna pesa wanakuja kuchukua pay day end month, mimi ni msukuma nadhani wote mnajua usukumani mtu mfupi kabisa ndie anaweza kushika namba moja kwa urefu hapa Dar,

Kwa kweli hadi nakuja kwenu nimejifanyia uchunguzi mpana wa mwonekano na kujiridhisha sina tatizo kabisa, kuna mtu mmoja kazini nilimshirikisha akasema huenda kwa kuwa kiswahili chako kwa mbaaaali kina accent ya kisukuma ndio maana mkeo anaona aibu kuwa na wewe, Ingawa akasema ni badi mtu anaetoka kanda ya ziwa anaewza kugundua maana ni kwa mbaali sana, nadhani asilimia kubwaDar tuna ongea kwa accent ya makabila yetu sasa sioni kwanini iwe shida.

Mmeshauri nikae nae kwa hekima na upole aweze kuniambia kwa nn hapendi kuwa na mm mbele ya watu na anakua uncomfortable, mara zote amejibu hana tatizo lolote kwamba najistukia tu

Hivyo basi kwa kuwa ni kweli tatizo lipo, na ninajisikia vibaya kuona sithaminiwi na sababu siambiwi (anapotezea kila nikimuuliza) sina njia nyingine iliyobaki kutatua tatizo hili, nimeona nitafute upendo huo unakopatikana ili niweze kuthaminiwa kama wengine

Kuanzia sasa nitatoka outing zote na faith, harusi, na kadhalika, na ugomvi ukitokea kati yake na dada yake nitaenda kumpangishia mtaani, kwanza mimi ndie nimemsomesha chuo hivyo walau nikiwa nae nitajifidia

Siwezi kudharaulika kiasi hiki wana jf, just imagine mwanzoni mwa December kulikua na family day ya NMB hakuniambia, akaichukua familia nzima na kudai wamealikwa sehemu, t shirt za family day akaenda kuwavisha watoto huko huko beach, nastuka mchana washikaji niliowaacha nmb wananipigia simu kuniuliza mbona tunaiona familia yako ww haupo? Nikashangaa kumbe wife hakutaka niende huko, nilijiuliza vitu vingi sana, tulisafiri kwenda likizo nikijuliza maswali mengi bila majibu

Baada ya hiyo simu, nikaenda kimya nikajificha sehemu nakunywa bia, namuona wife akiwa na staff wenzie men and women wakiwa na wenzao huku watoto wao wakicheza pembeni, nilijiuliza hivi mm nna shida gani? Usiku nilipomuhoji akawa anapepesa macho tu bila majibu ya maana, eti hakudhani kama ningependa kwenda
Nimehitimisha kwamba hanipendi, simuachi wala kumfukuza home, ila tu nitatoka na mdogo wake kama mke wangu kwenye starehe na kadhalika,

Nimechoka

Nb: sijawahi kuvaa nguo kama za koffi olomide, pia sijawahi kumshika kwa uzinzi
 
Last edited by a moderator:
Pole sana
tahadhari tu
umesema mkeo yupo NMB
na juzi NMB familly day alienda peke yake
na wewe uliwahi kufanya kazi NMB ukahamia bank ingine
wewe ni msukuma
shemeji anaitwa Faith...

Yaani hadi hapo tu mkeo huu ujumbe keshaupata..na huyo Faith yuko ubungo now akirudishwa kwao....

Nashauri usiweke details za hivi tena..
utasababisha hata mauaji next time
 
mkuu naona kutoka na mdogo wake unaweza ukafanya mambo yakawa complicated kuliko hata sasa hivi, mimi naona either umvumile na ukubaliane nae jinsi alivyo au uachane nae moja kwa moja, kukomoana sio kuzuri, kunasababisha pande zote mbili hasara kubwa
 
Pole sana
tahadhari tu
umesema mkeo yupo NMB
na juzi NMB familly day alienda peke yake
na wewe uliwahi kufanya kazi NMB ukahamia bank ingine
wewe ni msukuma
shemeji anaitwa Faith...

Yaani hadi hapo tu mkeo huu ujumbe keshaupata..na huyo Faith yuko ubungo now akirudishwa kwao....

Nashauri usiweke details za hivi tena..
utasababisha hata mauaji next time
Heeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
 
Pole sana
tahadhari tu
umesema mkeo yupo NMB
na juzi NMB familly day alienda peke yake
na wewe uliwahi kufanya kazi NMB ukahamia bank ingine
wewe ni msukuma
shemeji anaitwa Faith...

Yaani hadi hapo tu mkeo huu ujumbe keshaupata..na huyo Faith yuko ubungo now akirudishwa kwao....

Nashauri usiweke details za hivi tena..
utasababisha hata mauaji next time
Muache bana....
Mwenzio anataka kujimuvuzisha kwa shemejie
 
Mkuu pole na mkasa unaokutana nao, ni kweli mkeo hakupendi hata kidogo na hata ufanye nini hautakaa uwe comfortable na hayo maisha.

Ushauri wangu wa bure, chonde chonde, kama ni mwanamke wa kutoka naye tafuta mwingine kabisa kabisa na siyo huyo ndugu yake,

1. Ikija kujulikana kuwa unatembea na mdogo wake, tayari umegonganisha familia yake kwa kiasi kikubwa sana, tena sana.

2. Ikitokea mkaachana na mkeo (akiamua kuondoka kwa sababu ya wewe kutembea na mdogo wake) wewe binafsi hutakaa uwe na amani kwenye huo uhusiano, probably unaweza kuvunjika mara moja.

3. Ninaamini hata wazazi wako ukiwaeleza tatizo lililopo kati yako na mkeo hawatakuelewa kama tayari unatembea na mdogo wake, maana inaweza kugeuka kwamba mama alikuchukia toka zamani baada ya yeye kujua unatembea na mdogo wake

4. Ikija ikatokea mkasuruhishana, bado itakuwa ni ngumu kuisha kwa sababu mdogo mtu ataendelea kuwa around, angekuwa mtu wa mbali inakuwa rahisi sana kuyamaliza

Kwa hiyo mkuu kama huu uamuzi bado hujautekeleza achana nao kabisa, tafuta mwanamke mwingine nje, utapata anayekupenda kama huo ndo uamuzi pekee uliobaki.

ACHANA NA SHEMEJI YAKO KABISA, NI FEDHEHA KUBWA SANA.
 
Pole sana mkuu ,haya ni mambo mazito ila do what makes you comfortable
 
Pole sana
tahadhari tu
umesema mkeo yupo NMB
na juzi NMB familly day alienda peke yake
na wewe uliwahi kufanya kazi NMB ukahamia bank ingine
wewe ni msukuma
shemeji anaitwa Faith...

Yaani hadi hapo tu mkeo huu ujumbe keshaupata..na huyo Faith yuko ubungo now akirudishwa kwao....

Nashauri usiweke details za hivi tena..
utasababisha hata mauaji next time
duh limeshafukuta? amerudishwa kwao na mtoa mada au na wazazi?
 
Mkuu Fanya kile moyo na akili yako vinaona sawa, mimi binafsi nakuelewa sana, inaumiza na sometimes unaweza kujiona huna thamani kabisa mbele ya jamii.
 
Mmmhh hapana usifanye hivyo hasira hasara halafu we ni mwanaume matatizo kama hayo yanatatulika kama utatumia busara na hekima katika kulitatua hilo ikiwezekana kaa nae kikao na watu walio karibu yenu au hata wazazi kuliko uamuzi unaotaka kuchukua
 
katika mahusiano tunaambiwa kuwa mapenzi yananjia zake. Njia ambazo Ukitembea ndani yako kamwe hutajutia mahusiano Yako. Wengi wetu tumekuwa ni watumwa wa kuchagua bila kuangalia kuwa je tunao wachagua wapo katika zile njia sahihi ZInazotakiwa?
 
Tafuta demu mwingine achana na huyo Mdogo wake hapo ni balaa ndio unalolitafuta
 
Raphael niskitika kusema namuunga mkono mkeo unamatatizo makubwa yalopelekea mkeo kukukwepa.
Nilisoma uzi wako kwa makini nikakuhurumia, leo pia nimeusoma ndpo nkagundua tatizo lako.
Kama hutajali njoo pm.
Unaelekea kubaya zaidi.
Pm
 
Back
Top Bottom