Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,971
- 2,232
Wadau,
Kama nilivyowasilisha mada yangu hapo awali:
Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz na nikaahidi kutoa mrejesho wa mambo yatakavyokwenda.
Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wana JF wote waliochangia kwani michango yao hata kama ilikuwa ni hasi kwangu imenipa fundisho kubwa sana.
Wapo waliobeza kwamba hiyo ni stori ya kutunga kuna wakati mimi nikilala na kutamani kwamba nikiamka hilo swala ligeuke kuwa ni ndoto lakini haikuwahi kuwa hivyo na hakkika haitakuja kuwa hivyo.
Kuna wengine walioniona kwamba simpendi mke wangu ukweli ni kwamba nampenda sana mke wangu hilo limetokea si kwa kukusudia bali ni uzembe uliotokana na kutokuwa mwangalifu. Mtu aliye kaa Korea anajua kabisa wanawake wa Kikorea si rahisi kuwa na mahusiano na wageni hasa ngozi nyeusi, kwa kujua vile ukaribu na mchepuko huyu nilijua kabisa haututafika popote zaidi ya kuwa academic partiners.
Ghafla bin vuu tulijikuta tumeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, ilikuwa ni siku moja tu lakini tukajikuta tumejenga mazoea. Pamoja na kuingia kwenye mapenzi akili yangu siku zote ilikuwa inajua kuwa uhusiano huu ni wa muda kulingana na utofauti wa rangi zetu. Pasipo kujua mwenzangu akawa amekolea, nilikuja kugundua baadaye sana nami akawa taratibu kaingia moyoni, nikawa naogopa kumwambia asije akaumia nikamwona mbele yangu, kwa jinsi alivyokuwa amejitoa kwangu sikupenda kumuona akiwa na maumivu.
Michango ya wadau mbalimbali imenifanya ning'amue mambo yafuatayo:
1. Kwamba kosa nilililolifanya ni aibu si kwangu tu bali ni kwa watanzania wote.
2. Kwamba kitendo cha kutokuweka wazi hali yangu ya kindoa ndiyo kimesababisha matatizo yote haya.
3. Kwamba iwapo nitakurupuka na kuweka wazi swala la kuachana naye nikiwa kwenye ardhi ya Korea kuna hatari ya kushindwa kutoka salama.
4. Kwamba mkorea anaweza kujidhuru iwapo nitamtoroka nikiwa nimemwachia ujauzito hii inaweza kupelekea mimi kupata laana au pengine familia wakaamua kulifuatilia hilo swala.
5. Kwamba mkorea hawezi kuishi kwa amani akiwa na mtoto aliyezaa na ngozi nyeusi na mwanangu anaweza kuwa na maisha magumu sana.
6. Kwamba nitafanya makosa sana iwapo nitaachana na mke wangu kwa sababu ya mkorea.
a. Sitamweleza mkorea mpaka nimefika Tz kwa hiyo nitakuja naye Tz tukifika nitampangia nyumba mbali na familia yangu ilipo. Nitatafuta siku maalum ya kumweleza na nitamweleza kwamba sikuwahi kukuambia kwa sababu ya mapenzi niliyonayo kwako na nilihofia ningelikwambia usingekubali kuwa nami wala usingelikubali kuja Tz. Najua kwa wivu alionao atachachamaa na pengine atataka kurudi kwao. Vurugu zote atakazofanya mimi nitakuwa salama kwa sababu nitakuwa nipo uwanja wa nyumbani " home grounds"
b. Familia yangu sitaiambia tarehe sahihi ya kurejea ili niweze kukamilisha shughuli za kumhifadhi mkorea. Pia kama ni zawadi za mke wangu na watoto naweza kuzinunua hata Kariakoo.
c. Kuanzia sasa nitajitahidi kuweka wazi kwamba nimeoa ili kuepusha mahusiano yasiwe rasmi.
d. Baada ya kumweleza Mkorea nitamweleza na mke wangu, maana nitakuwa nimepata respond ya mkorea. Nitamwangukia mke wangu anisamehe kwa aibu niliyosababisha. Mkorea akitaka kuendelea nami nitamwambia kwamba tufanye siri mana mimi mume wa mtu vinginevyo anaweza kuingia kwenye matatizo ya kuingilia ndoa.
e. Iwapo ataamua kubaki Tz nitamfanyia mpango wa kupata uraia na pia kumshauri afungue mradi wa kuzalisha pesa ili aweze kujiingizia kipato.
f. Naomba msamaha kwa watanzania wote fedheha niliyoisababisha kwenu.
Uamuzi huu nimefikia baada ya kupata ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wapo waliokuja mpaka inbox na kunishauri. Nimezingatia ukweli usemao kwamba;
"Akili za kuambiwa changanya na za kwako." Sitalaumu mtu kwa yatakayonipata, mamuzi ni yangu.
Kama nilivyowasilisha mada yangu hapo awali:
Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz na nikaahidi kutoa mrejesho wa mambo yatakavyokwenda.
Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wana JF wote waliochangia kwani michango yao hata kama ilikuwa ni hasi kwangu imenipa fundisho kubwa sana.
Wapo waliobeza kwamba hiyo ni stori ya kutunga kuna wakati mimi nikilala na kutamani kwamba nikiamka hilo swala ligeuke kuwa ni ndoto lakini haikuwahi kuwa hivyo na hakkika haitakuja kuwa hivyo.
Kuna wengine walioniona kwamba simpendi mke wangu ukweli ni kwamba nampenda sana mke wangu hilo limetokea si kwa kukusudia bali ni uzembe uliotokana na kutokuwa mwangalifu. Mtu aliye kaa Korea anajua kabisa wanawake wa Kikorea si rahisi kuwa na mahusiano na wageni hasa ngozi nyeusi, kwa kujua vile ukaribu na mchepuko huyu nilijua kabisa haututafika popote zaidi ya kuwa academic partiners.
Ghafla bin vuu tulijikuta tumeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, ilikuwa ni siku moja tu lakini tukajikuta tumejenga mazoea. Pamoja na kuingia kwenye mapenzi akili yangu siku zote ilikuwa inajua kuwa uhusiano huu ni wa muda kulingana na utofauti wa rangi zetu. Pasipo kujua mwenzangu akawa amekolea, nilikuja kugundua baadaye sana nami akawa taratibu kaingia moyoni, nikawa naogopa kumwambia asije akaumia nikamwona mbele yangu, kwa jinsi alivyokuwa amejitoa kwangu sikupenda kumuona akiwa na maumivu.
Michango ya wadau mbalimbali imenifanya ning'amue mambo yafuatayo:
1. Kwamba kosa nilililolifanya ni aibu si kwangu tu bali ni kwa watanzania wote.
2. Kwamba kitendo cha kutokuweka wazi hali yangu ya kindoa ndiyo kimesababisha matatizo yote haya.
3. Kwamba iwapo nitakurupuka na kuweka wazi swala la kuachana naye nikiwa kwenye ardhi ya Korea kuna hatari ya kushindwa kutoka salama.
4. Kwamba mkorea anaweza kujidhuru iwapo nitamtoroka nikiwa nimemwachia ujauzito hii inaweza kupelekea mimi kupata laana au pengine familia wakaamua kulifuatilia hilo swala.
5. Kwamba mkorea hawezi kuishi kwa amani akiwa na mtoto aliyezaa na ngozi nyeusi na mwanangu anaweza kuwa na maisha magumu sana.
6. Kwamba nitafanya makosa sana iwapo nitaachana na mke wangu kwa sababu ya mkorea.
Maamuzi:
Kutokana na mambo yaliyoainishwa hapo juu nimeamua yafuatayo:a. Sitamweleza mkorea mpaka nimefika Tz kwa hiyo nitakuja naye Tz tukifika nitampangia nyumba mbali na familia yangu ilipo. Nitatafuta siku maalum ya kumweleza na nitamweleza kwamba sikuwahi kukuambia kwa sababu ya mapenzi niliyonayo kwako na nilihofia ningelikwambia usingekubali kuwa nami wala usingelikubali kuja Tz. Najua kwa wivu alionao atachachamaa na pengine atataka kurudi kwao. Vurugu zote atakazofanya mimi nitakuwa salama kwa sababu nitakuwa nipo uwanja wa nyumbani " home grounds"