Mrejesho kuhusu SADC hapa Tanzania

Mrejesho kuhusu SADC hapa Tanzania

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu habari za jioni, kama wiki mbili zilizopita niliomba msaada wa kuoneshwa zilipo ofisi za jumuiya ya kiuchumi ya Nchi za kusini Mwa jangwa la sahara SADC hapa Tanzania,
Kuna mdau alinipa namba ya simu na anuani yao akinisihi pia nilete mrejesho hapa.
Wakuu, kama nilivyosema awali katika Malalamiko yangu, ! Ama ofisi hii ni ya ubabaishaji au sisi Watanzania hatuko serious (makini) na masuala haya..
Nimesema haya kwa namna nilivyopata taabu ya kupata mawasiliano na wahusika wa ofisini hizi..
Kwanza niliambiwa niende water front. Nikipewa na namba za simu ambazo kiukweli zilikuwa hazipokelewi,
Nilipofika water Font walinzi wakaniambia tangu ofisi hizo zihame hapo ni miaka sita iliyopita.na hawajui wako wapi.
Nikaomba msaada police makao makuu wakaniambia ofisi zao zilikuwa Pale jengo la kitega uchumi,
Nikaenda pale meneja wa lile jengo akanijulisha hawako hapo, tangu waondoke ni miaka minne. Imepita..
Nikaambiwa nijaribu wizara ya mambo ya nje, pale kivukoni,
Napo wakaniambia hawajui chochote huenda wamehamia Dodoma.
Nikapewa namba ya mtu wa Sadc Dodoma.
Tangu nianze kumpigia huyu mtu ni wiki ya pili sasa hajawahi pokea hata siku moja, pamoja na kumtumia ujumbe mfupi sikuwahi pata jibu lolote,
Ninatamani kuweka namba yake ya simu hapa lakini nadhani haitakuwa kitendo cha kiungwana.!
Baada ya changamoto hizi nimejiuliza maswali haya yafutayo.

1: Endapo mimi Mtanzania niliye hapa Dar es Salaam napata shida kwa kiwango hiki kupata tu taarifa muhimu za Sadc vip kuhusu mtu anayetoka mkoani..?

2: kama hii jumuiya ipo kama ambavyo tunaona viongozi wetu wakihudhuria vikao je ipo kwa manufaa ya watu wa aina gani?

3: huku mwisho napatwa tu na hasira maana nikiendelea kuuliza nitatukana.

Nawasilisha..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukana tu mkuu vitu vingine vinakera , MODS watakusamehe tu.
 
Tukana tu mkuu vitu vingine vinakera , MODS watakusamehe tu.
Mkuu kwa ujazo wa fukuto lililo ndani yangu ntakalolitamka linaweza baadae kunisumbua hata mimi mwenyewe,
Haiwezekani mtu unakaa kwenye ofisi ya umma, unapokea mshahara na marupuru yote, unahudhuria vikao ndani na Nje ya Nchi wakati kiuhalisia nyie ni wahuni.

HIVI MTU AMBAYE SIO RAIA WA NCHI YETU UNATEGEMEA ANGESEMA NINI BAADA YA USUMBUFU WA KIWANGO HIKI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana mimi huwa nasemaga Tanzania sio sehemu sahihi ya kuishi kwa mtu mwenye akili timamu na uwezo wa kuishi sehemu nyingine anao. Nasema haya japo naonekana tahira ila wengi wenye akili zao timamu huwa wananielewa na kuniunga mkono ninachokisema.

Watu hawathamini muda wala malengo ya mtu, pengine labda wewe ungeweza kuleta wawekezaji hapa nchini kwa kuwapa taarifa zenye ushawishi kuhusiana na nchii hii kupitia hiyo trip yako uliyoiandaa, lakini kwa sababu ubini wako pengine haujawahi kuskika kwenye taasisi yoyote kubwa basi unapuuzwa tu.

OVYO SANA HII NCHI
 
Mkuu kwa ujazo wa fukuto lililo ndani yangu ntakalolitamka linaweza baadae kunisumbua hata mimi mwenyewe,
Haiwezekani mtu unakaa kwenye ofisi ya umma, unapokea mshahara na marupuru yote, unahudhuria vikao ndani na Nje ya Nchi wakati kiuhalisia nyie ni wahuni.

HIVI MTU AMBAYE SIO RAIA WA NCHI YETU UNATEGEMEA ANGESEMA NINI BAADA YA USUMBUFU WA KIWANGO HIKI?

Sent using Jamii Forums mobile app

THIS IS TANZANIA [emoji1241] MY BROTHER.
 
aisee pole sana, nimechungulia nondo zangu hapa ni kweli kuna tatizo. Yani sikutegemea ingekua serious hivi.
 
Ni kweli kabisa sisi (hasa watumishi wa umma) hatupo makini kujali na kuthamini mahitaji ya wengine sijui tuna tatizo gani huwa nakereka sana napotumia gharama (isiyo ya lazima) kutafuta huduma ambayo ni haki ya kirai ila basi tu hamna namna.
 
aisee pole sana, nimechungulia nondo zangu hapa ni kweli kuna tatizo. Yani sikutegemea ingekua serious hivi.
Ajabu ni vipi viongozi wetu wanaenda kuhudhuria vikao na mikutano ambayo wao hawana ofisi kwa ajili ya wananchi wao hapa nyumbani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi nadhani mengine wa kujilaumu ni wewe. WaTanzania wengi tuna hulka ya kulaumu bila kufanya research. Kosa kubwa!

SADC ni shirika la kikanda. Inter regional organization. Hakika Foreign Affairs/Wizara ya Mambo ya Nje wanajua SADC ofisi zao ziko wapo. Kwa sababu KAMA wana ofisi Tanzania, wana hadhi ya kibalozi. SADC siyo NGO kwamba unaweza kuitafuta kwa tochi. Hata pale Foreign kuna uwezekano tena mkubwa kwamba kuna desk ofisa anayeshughulikia mashirika ya kikanda likiwemo SADC. Kwa hiyo ungeweza kwenda ukamuuliza vizuri angekwambia kama wapo Tanzania au hawapo. Katika Mashirika yanayojielewa mojawapo ni SADC. Mkuu ile siyo NGO!

Kama ungekosa kabisa unge-google au ukauliza SADC makao makuu kwa email au kwa simu. Kwa mfano ukiuliza google unapata hii:

Tanzania SADC National Contact Point
Mr. Innocent E Shiyo,
SADC National Contact Point
Acting Director,
Department of Regional Cooperation,
Ministry of ForeignAffairs and International Cooperation
P.O. Box 9000,
DAR ES SALAAM,
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
.
Tel : (+255) 22 2120532
Fax : (+255) 22 2120529
Mobile : (+255) 784 511 626
Email: shiyo27@yahoo.co.uk
CC: drc@foreign.go.tz

Huyu bwana Shiyo ni Balozi na yuko pale Foreign Affairs! Sasa wewe ndugu yangu ulienda kutafuta information wapi? Mimi naona ulitumia nguvu kubwa kuliko weledi katika kufanikisha hili jambo.

Next time, jitahidi kutumia weledi zaidi kufanikisha mambo ya muhimu kama haya.
 
Ndugu mpaka nimeamua kulileta hapa jukwaani sijakurupuka, hata hivyo ni hulka ya watumishi wengi wa umma wa Tanzania kutumia maelezo kama yako hasa pale wanapoona ama habari zao ziko bayana au kuna hatari ya kubainishwa kwa mapungufu ya ofisi zao.
Hiyo anuani uliyonipa nimepewa na watu zaidi ya watatu katika ofisi nilizo pita nikitafuta mawasiliano na wahusika wa SADC hapa Tanzania..
Sikukurupuka sabbu hata hizo simu za mkononi walionipa ni hao niliowakuta huko unako nielekeza ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom