Mrejesho kuhusu SADC hapa Tanzania.

Mrejesho kuhusu SADC hapa Tanzania.

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu habari za jioni, kama wiki mbili zilizopita niliomba msaada wa kuoneshwa zilipo ofisi za jumuiya ya kiuchumi ya Nchi za kusini Mwa jangwa la sahara SADC hapa Tanzania,
Kuna mdau alinipa namba ya simu na anuani yao akinisihi pia nilete mrejesho hapa.
Wakuu, kama nilivyosema awali katika Malalamiko yangu, ! Ama ofisi hii ni ya ubabaishaji au sisi Watanzania hatuko serious (makini) na masuala haya..
Nimesema haya kwa namna nilivyopata taabu ya kupata mawasiliano na wahusika wa ofisini hizi..
Kwanza niliambiwa niende water front. Nikipewa na namba za simu ambazo kiukweli zilikuwa hazipokelewi,
Nilipofika water Font walinzi wakaniambia tangu ofisi hizo zihame hapo ni miaka sita iliyopita.na hawajui wako wapi.
Nikaomba msaada police makao makuu wakaniambia ofisi zao zilikuwa Pale jengo la kitega uchumi,
Nikaenda pale meneja wa lile jengo akanijulisha hawako hapo, tangu waondoke ni miaka minne. Imepita..
Nikaambiwa nijaribu wizara ya mambo ya nje, pale kivukoni,
Napo wakaniambia hawajui chochote huenda wamehamia Dodoma.
Nikapewa namba ya mtu wa Sadc Dodoma.
Tangu nianze kumpigia huyu mtu ni wiki ya pili sasa hajawahi pokea hata siku moja, pamoja na kumtumia ujumbe mfupi sikuwahi pata jibu lolote,
Ninatamani kuweka namba yake ya simu hapa lakini nadhani haitakuwa kitendo cha kiungwana.!
Baada ya changamoto hizi nimejiuliza maswali haya yafutayo.

1: Endapo mimi Mtanzania niliye hapa Dar es Salaam napata shida kwa kiwango hiki kupata tu taarifa muhimu za Sadc vip kuhusu mtu anayetoka mkoani..?

2: kama hii jumuiya ipo kama ambavyo tunaona viongozi wetu wakihudhuria vikao je ipo kwa manufaa ya watu wa aina gani?

3: huku mwisho napatwa tu na hasira maana nikiendelea kuuliza nitatukana.

Nawasilisha..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikate tamaa, the change is you and me , this is our country and the changes you are dreaming of, are within us all! Pole sana!
 
Back
Top Bottom