bobby bwana harusi
New Member
- May 17, 2016
- 3
- 35
Wadau habari za Muda mrefu,
Mwaka juzi niliwaletea kisa kilichonitokea fuata link hiyo Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi, naomba niwakumbushe kwa muktasari.
Mwaka juzi, siku moja nilipigiwa simu kuwa mama kule mkoani anaumwa sana na amepewa rufaa kuja Muhimbili, akaletwa, huduma Muhimbili zilikuwa ni za kusuasua sana, nikampeleka Agakhan, nikaambiwa utaratibu ni ku deposit 1.5 million ili awe admitted na alitakiwa kufanyiwa operation siku hiyo au kesho yake ikizidi sana.
Kwa kuwa jambo hilo lilinikuta off guard sikuwa na pesa kabisa, nilikua ndio nimetoka kununua kiwanja karibu 10 milion, nikalazimika kumuomba mchumba wangu msaada, kwa kuwa tulikuwa tunafanya kazi pamoja katika benki, nilichungulia akaunti yake kwanza na kuona ina pesa nyingi tu karibu mara tano ya kiwango nilichohitaji, ndipo nikamueleza, alikuwa anajua kuhusu mama kuwepo mjini kwa matibabu, kinyume na matarajio alidai hana hata senti tano kwenye akaunti akanishauri niombe mkopo wa dharura hapo kazini.
Anyway kwa kifupi nilisaidiwa na msichana mwingine hapo kazini ambae tumefanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mimi niliingia hapo 2004 yeye 2009, mchumba wangu ninaemzungumzia hapa ndio kwanza alikuwa amemaliza kama miezi nane hivi kazini na hapo alikuwa trainee wangu.
Baada ya mzazi wangu kupona niliamua kuvunja uchumba na huyo msichana wangu alienitupa wakati wa shida, jambo hilo lilileta mgogoro mkubwa sana maana hadi navunja uchumba tulikuwa tumeshalipa mahari, pande zote tulikuwa tunatarajia kuanza vikao Muda si mrefu.
Pamoja na jitihada zote za usuluhishi mimi na familia yangu tulikataa kabisa kuendelea na harusi, pamoja na binti kunililia na kuniomba msamaha nilikataa kata kata maana MUNGU ameniepusha na binti huyu ambae yuko radhi mama yangu afe wakati ana hela za kusaidia kwenye akaunti yake, na mimi nimeshamsaidia sana huko nyuma tena kwa vitu vya anasa.
Wengi mlinishauri nichukue Muda wa kutosha kurudi kwenye mahusiano kutokana na yaliyonikuta, kwa kuwa niliamini ni MUNGU ndie amemtumia yule work mate mwingine kunisaidia, niliamua kutii sauti ya MUNGU, niliamwambia yule binti jiandae nakuoa wewe.
Mimi nilikuwa tayari kuacha tarehe ya harusi ibaki ile ile ya awali ila bibi harusi ndio awe huyu mpya, lakini wazee na bosi wangu kazini akasema italeta picha mbaya na uhasama mkubwa kati ya mabinti hao wawili na koo zetu kwa ujumla, hivyo tukaamua kuwa wachumba kwanza tukifanya taratibu zingine hata hivyo wote mimi na mchumba wangu tulihama benki hiyo Muda tu na mashirika tofauti.
Mwezi wa Tatu mwaka huu tulifunga ndoa, nimeitafuta sana password ya akaunti yangu ya JF bila mafanikio, wakati mwingine wanadai hata username pia nimekosea, wakati mambo haya yanatokea ndio nilikuwa nimefungua akaunti JF hivyo ilikuwa mpya.
Nimelazimika kufungua akaunti mpya ili nirudishe shukrani zangu kwenu, maana zaidi ya wachangiaji 400 kama sikosei mlitoa ushauri kwamba nini nifanye na kipi nisifanye.
Nimefahamu kuwa kila jambo linatokea kwa sababu maalum, namshukuru MUNGU kwa yote, baada ya kuhama kazi mambo yangu yalikwenda vizuri sana kiasi cha kujiuliza kwa nini nimedumu pale tangu 2004 hadi 2014, nimekimbizana na Muda, tulipotoka honeymoon hatukurudi kwenye kupanga tena, tumepitiliza kwetu moja kwa moja, finishing itafanyika taratibu, lakini vitu vyote vya matumizi ya binadaam vipo.
Asanteni.