Mradi wa upandaji miti wilaya ya Hai wafanikiwa kwa asilimia kubwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Mradi wa upandaji miti ndani ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambalo Mbunge wake ni Mhe. Freeman Mbowe, ulianza mwaka 2012 na umefanikiwa kwa asilimia kubwa ingawa bado zipo changamoto mbalimbali.

Mradi huo wa upandaji umefanikiwa kupanda miti pembezoni mwa barabara za Hai kwa umbali wa kilomita 47 kuanzia unapoanza kuingia Wilaya ya Hai kutoka Moshi mjini hadi Machame, Kutokea Boma hadi mpakani mwa Hai na Sanya juu, na kutoka Boma mpaka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Kutoka Boma hadi njia panda ya KIA kumekuwa na changamoto kwa wafugaji kuachia mifugo yao kula miti pindi inapokuwa midogo, pia hujuma zenye muonekano wa kisiasa kwa sababu viongozi wa maeneo hayo wanaona bila Kuchukua hatua dhidi ya wale wanaohujumu mradi huo na Tanesco kupitisha nguzo za umeme juu ya miti hiyo ikiwa wameikuta miti, haihitaji Diploma kujua usogee pembeni hatua kadhaa kupisha miti hiyo kwa sababu ikikuwa lazima itagusa waya na kutakiwa kukatwa.

IMG-20160715-WA0085.jpg

Mradi huu endelevu lengo ni kupanda miti Milioni 3, yakiwemo maeneo ya pembezoni mwa barabara za Wilaya ya Hai, vyanzo vya maji, mabonde ya mito na maeneo ya tambarare.

Lengo la kupanda miti hii ni kupunguza hali ya jangwa inayozikabili baadhi ya sehemu katika Wilaya ya Hai, kupendezesha mazingira na kutoa vivuli kwa wanaotembea pembeni ya barabara, pamoja na kuzuia mmomonyoko wa ardhi unaoweza kujitokeza wakati wa mvua na kuharibu barabara.

Kusaidia kupunguza
ongezeko la joto (Global Warming) pamoja na hali ya kubadilikabadilika kwa hali ya hewa yani tabia nchi.

Changamoto ni kubwa idadi ya ukataji miti haiendani na idadi ya upandaji miti nchini,Serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka bila kufanya hivyo nchi yetu inakwenda kuwa na sehemu kubwa ambayo ni jangwa.

Wananchi pia wanatakiwa kuilinda miti ambayo imeshapandwa isiharibiwe na binadamu wala wanyama kwani ni kwa manufaa ya kila mmoja wetu.
 
Hongera mheshimiwa sasa una ile programme ya kilimo cha mboga,ili kukuza kipato cha wananchi naomba usiache.....pambana soon wakati kule mtera wanakutukana kuwa unaisoma namba sis tutakuwa tunazidi jenga nyumba za block...
 
Kipaumbele cha Hai siyo hiyo miti .Cha muhimu cha kwanza ahakikishe halmashauri ya Hai haipati hati chafu kwenye ukaguzi wa CAG
 
Mradi wa upandaji miti ndani ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambalo Mbunge wake ni Mhe. Freeman Mbowe, ulianza mwaka 2012 na umefanikiwa kwa asilimia kubwa ingawa bado zipo changamoto mbalimbali.

Mradi huo wa upandaji umefanikiwa kupanda miti pembezoni mwa barabara za Hai kwa umbali wa kilomita 47 kuanzia unapoanza kuingia Wilaya ya Hai kutoka Moshi mjini hadi Machame, Kutokea Boma hadi mpakani mwa Hai na Sanya juu, na kutoka Boma mpaka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Kutoka Boma hadi njia panda ya KIA kumekuwa na changamoto kwa wafugaji kuachia mifugo yao kula miti pindi inapokuwa midogo, pia hujuma zenye muonekano wa kisiasa kwa sababu viongozi wa maeneo hayo wanaona bila Kuchukua hatua dhidi ya wale wanaohujumu mradi huo na Tanesco kupitisha nguzo za umeme juu ya miti hiyo ikiwa wameikuta miti, haihitaji Diploma kujua usogee pembeni hatua kadhaa kupisha miti hiyo kwa sababu ikikuwa lazima itagusa waya na kutakiwa kukatwa.

View attachment 366490

Mradi huu endelevu lengo ni kupanda miti Milioni 3, yakiwemo maeneo ya pembezoni mwa barabara za Wilaya ya Hai, vyanzo vya maji, mabonde ya mito na maeneo ya tambarare.

Lengo la kupanda miti hii ni kupunguza hali ya jangwa inayozikabili baadhi ya sehemu katika Wilaya ya Hai, kupendezesha mazingira na kutoa vivuli kwa wanaotembea pembeni ya barabara, pamoja na kuzuia mmomonyoko wa ardhi unaoweza kujitokeza wakati wa mvua na kuharibu barabara.

Kusaidia kupunguza
ongezeko la joto (Global Warming) pamoja na hali ya kubadilikabadilika kwa hali ya hewa yani tabia nchi.

Changamoto ni kubwa idadi ya ukataji miti haiendani na idadi ya upandaji miti nchini,Serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka bila kufanya hivyo nchi yetu inakwenda kuwa na sehemu kubwa ambayo ni jangwa.

Wananchi pia wanatakiwa kuilinda miti ambayo imeshapandwa isiharibiwe na binadamu wala wanyama kwani ni kwa manufaa ya kila mmoja wetu.

Nasi tunatekeleza mtwara for three years tutapanda miti laki tatu
 
Kipaumbele cha Hai siyo hiyo miti .Cha muhimu cha kwanza ahakikishe halmashauri ya Hai haipati hati chafu kwenye ukaguzi wa CAG
Hilo limefanyika watumishi 6 walifukuzwa kazi....ila sasa tunakuza uchumi......mradi mkubwa wa kilimo cha mbogamboga umeanza tutawauzia mpaka kule ....chato mboga
 
Juzi kati nilitembelea ukanda wa huko - Moshi to Arusha. To my surprise, nilishangaa kuona kilele cha Mawenzi hakina hata mfano wa theluji pamoja na kwamba huu ni msimu wa baridi kali. Enzi zile kipindi kama hiki Mawenzi ingekuwa imefurika theluji. Kibo nayo theluji imebaki kidogo sana at the top tofauti na miaka ya nyuma. Waliotabiri by 2030 theluji itakuwa historia Mt. Kilimanjaro kweli ni wabobezi!
 
Back
Top Bottom