Mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) mwaka wa 2008

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
Baada ya matatizo yaliyoniandama katika vitabu hivyo viwili nilivyoandika siku moja mwaka wa 2008 nikapokea email kutoka kwa Prof. Emmanuel Akyeampong kutoka Harvard akaniomba niwe mmoja wa waandishi karibu 500 kutoka kila pembe ya dunia watakaoandika kamusi ya watu mashuhuru Afrika.

Mradi huu ulikuwa unajulikana kama Dictionary of African Biography.
Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Prof. Akyeampong akaniomba pia niwe mshauri wake kwa majina ya Watanzania ambao mimi naona wamefanya makubwa kwa hiyo wanastahili maisha yao kuandikwa katika hii kamusi.

Prof. Akyeampong akaniomba mimi niandike maisha ya Kleist Sykes yeye akimkusudia Kleist Abdulwahid Sykes.

Mimi hapo hapo nikaanza kazi yangu ya ushauri.

Nikalikata jina la Mayor wa Jiji la Dar es Salaam rafiki na ndugu yangu Kleist, nikamshauri Prof. Akyeampong kuwa anaestahili kuingia katika DAB ni babu yake, Kleist Sykes Mbuwane (1894 - 1949) na si huyu Kleist mtoto wa Abdul Sykes.

Prof. Akyeampong alivutiwa sana na kile alichosoma kuhusu babu yake Kleist Abdulwahid na kamusi ilipochapwa mwaka wa 2011 maisha ya Kleist Sykes Mbuwane babu yake Kleist Abdulwahid yakawa ndani ya DAB.

DAB ina volume sita na ni maarufu hivi sasa duniani kama kitabu vya rejea kwa watu mashuhuri na mashujaa wa Bara la Afrika.
 
...katika Tanzania yote ni hilo moja tu (Kleist Sykes Mbuwane) uliloshauri liingizwe kwenye DAB au kuna mengine? Kama yapo orodhesha hapa na toa justification tafadhali.
 
... katika Tanzania yote ni hilo moja tu (Kleist Sykes Mbuwane) uliloshauri liingizwe kwenye DAB au kuna mengine? Kama yapo orodhesha hapa na toa justification tafadhali.

I'm longing kusikia majina aliyoshauri mkuu Mohamed hasa tokana na mrengo wake.
 
Mimi ningependa historia ya jina la Ilala.anbayo kwa sasa ndii wialaya ya Ilala
 
...katika Tanzania yote ni hilo moja tu (Kleist Sykes Mbuwane) uliloshauri liingizwe kwenye DAB au kuna mengine? Kama yapo orodhesha hapa na toa justification tafadhali.
Dudus,
Kuna jina la Julius Nyerere katika DAB, Joseph Merinyo kwa kuyataja machache.

Majina niliyoletewa yalikuwa mengi lakini nililoshughulikia mwanzo lilikuwa la Kleist Abdul Sykes nikapendekeza litolewe awekwe babu yake Kleist Sykes Mbuwane.

Sababu niliyowapa ni kuwa Kleist hakufanya makubwa aliyofanya babu na baba zake.
 
...katika Tanzania yote ni hilo moja tu (Kleist Sykes Mbuwane) uliloshauri liingizwe kwenye DAB au kuna mengine? Kama yapo orodhesha hapa na toa justification tafadhali.
Ndugu yangu Dudus nakuhurumia.

Unadhani mimi ni mtu wa maskhara?

Hivi umeingia upofu kiasi unashindwa kuukubali ukweli?

Unadhani Harvard na Oxford ni watu wa kutaniwa?

Unaujua mchujo uliopita hadi jina langu kupitishwa?

Fanya utafiti kidogo basi angalau unifahamu.

Hivi unajua Oxford wameshaniingiza katika miradi yao mingapi?
 
Babu haujaeleza vizuri kazi yako hiyo ilikua na mipaka gani; ulitaja tu na kukata majina au uliyatafiti na kuwekwa kitabuni?

Mzee Philip Mangula yumo?
 
Babu haujaeleza vizuri kazi yako hiyo ilikua na mipaka gani; ulitaja tu na kukata majina au uliyatafiti na kuwekwa kitabuni?

Mzee Philip Mangula yumo?
Kila...
Ukitaka kuelewa mantiki ya hii post inakubidi uanze kusoma yale niliyoeleza baada ya vitabu vyangu viwili kukutwa na matatizo - ''The Torch on Kilimanjaro,'' na ''Uamuzi wa Busara.''

Nilikabidhiwa majina mengi sana lakini siwezi kuyataja kwani haitapendeza.

Mwisho ukipenda kuniita kwa umri wangu sawa.

Ukiniita babu unakuwa unapoteza haiba yangu na yako kwani wewe ni mkubwa huwezi kuwa mjukuu wangu.

Nina wajukuu wadogo sana kwako wanaweza kuwa wanao kwa hiyo mimi ni umri wa baba yako.

Ukipenda niite baba kwa kuwa wajukuu zangu wanaoniiita babu nikiwafananisha na wewe hamlingani kwa mbali sana.

Katika mila zetu majina kwa kufuata nasaba na umri yana maana kubwa sana.
 
...katika Tanzania yote ni hilo moja tu (Kleist Sykes Mbuwane) uliloshauri liingizwe kwenye DAB au kuna mengine? Kama yapo orodhesha hapa na toa justification tafadhali.
Si unaona kabisa mkuu DAB yani umeshamsahau katumbuliwa juzi tu alikua ni Khalifa wa hapo Mzizima?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom