MRADI BOMBA LA MAFUTA WASHIKA KASI

MRADI BOMBA LA MAFUTA WASHIKA KASI

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
download.jpg



MRADI wa kusarisha mafuta gha kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania umeshika kasi baada ya Tanzania kuanza utekelezaji katika hatua mbalimbali huku majadiliano ya ndani kwa nchi yakikamilika Januari mwakani. Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amesema hayo baada ya kikao cha mawaziri wa sekta zinazosimamia mradi kwa nchi za Uganda na Tanzania kuwa utekelezaji wa mradi huo haujasimama. Mkutano huo wa ngazi ya mawaziri, ulihudhuriwa pia na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na mawaziri wa Uganda kutoka sekta zinazoshiriki katika mradi walihudhuria.

Amesema hatua zilizokiwa katika utekelezaji wa mradi kwa upande wa Tanzania tayari wamekamilisha utati wa kijiolojia na kijiozikia na sasa wanaendelea na uchimbaji wa mashimo ambamo bomba hilo la mafuta litalazwa. Aidha amesema uchimbaji mashimo umeshafanyika katika mikoa ya Tanga na Manyara na sasa inaendelea katika Mkoa wa Dodoma, wilayani Kondoa. Vilevile alieleza kwamba tathmini zote za mazingira zimekamilika, taratibu za masuala ya fidia na ustawi wa jamii ambapo mradi utapita zimekamilika na hatua inayofuata sasa baada ya majadiliano kukamilika ni ujenzi. Waziri Kalemani alibainisha kuwa mradi haujachelewa kwani unatekelezwa hatua kwa hatua.

“Naomba mkawaeleze wananchi wa pande zote kuwa utekelezaji wa mradi huu haujasimama, kimsingi tunaanza kwa nguvu kubwa kuutekeleza ili ukamilike kama tulivyopanga,” alisema na kuongeza kuwa mwaka jana ulisainiwa mkataba, yakapatikana maeneo, kutoa dia upande wa Tanga, kukamilisha utati wa mazingira, kufahamu ukubwa wa bomba, na sasa kuanza kuchimba mashimo ambapo bomba litalazwa.

Amesema Januari 17 mwakani utakapofanyika mkutano kama huo nchini Uganda wamekubaliana kukamilisha majadiliano ambayo lazima yake kwa manufaa ya nchi kama kwa upande wa Tanzania, kuainisha kampuni mbalimbali za ndani ili kuzijengea uwezo na kubainisha utaratibu wa namna ya kuzishirikisha ziweze kunufaika na mradi husika.

Aidha, amesema ziko jamii za watanzania ambazo zinalengwa zinufaike na mradi husika na kwamba yako mapato yatokanayo na mradi ambayo yanapaswa yaingie kwenye Pato la Taifa, hivyo ni lazima majadiliano yazingatie taratibu zote ili mradi uwe wa manufaa.

Waziri Kalemani amesema majadiliano ya pande hizo mbili yalikuwa chini ya Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni na walikubaliana kuwa kila nchi ihakikishe inamaliza majadiliano kwa muda uliopangwa.

Akieleza hatua iliyokiwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa Tanzania alisema kwa sasa wamekamilisha maandalizi ya utati wa kijiolojia, utati wa kijiozikia na sasa wanaendelea na uchimbaji wa mashimo kwa kwenda katika mikoa mitatu na tayari wamemaliza Tanga, Manyara na sasa Kondoa mjii Dodoma. Amesema hatua za awali za utekelezaji zimeanza kwa kukamilisha tathmini za mazingira, dia na ustawi wa jamii imekamilika katika mradi utakapopita na kinachofuata ni ujenzi baada ya majadiliano kukamilika. Waziri Kalemani alisema utekelezaji wa mradi uko katika hatua nyingi umeanza kwa kusaini mkataba, kupata maeneo, kudia kwa upande wa Tanga, utati wa mazingira, kubaini ukubwa wa bomba, kuchimba mashimo ambapo bomba litalala hivyo utekelezaji haujachelewa.

Waziri Muloni alisema wamekubaliana kuharakisha mchakato wa hatua za maandalizi ili ujenzi ufanyike kwa wakati na kuwanufaisha wananchi wa nchi zote mbili kama ilivyokusudiwa. Alisema mpaka sasa bado hawajakamilisha suala la uwekezaji kifedha, wanaendelea na majadiliano ili kukubaliana na wawekezaji,wanawasiliana na makampuni ili kukamilisha matarajio yao ya kutumia bomba.
 
Back
Top Bottom