Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,941
- 1,011
Habari ya asubuhi wanajamiiforums!
Baada ya kusheherekea Sikukuu za Christmass na Boxing Day, natumaini leo mu wazima kabisa.
Kwa waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam au wale waliokuwa na ukaribu na wanachuo wa Mlimani, kusikia jina la PUNCH haikuwa kitu kigeni.
Nikiwa Mtwara, niliwahi kukutana na mtu ambaye katika utu uzima wake(uzee), alikuwa ni mchoraji mzuri wa vikaragosi. Kuna Bwana mmoja alikuwa anafanyia Ujenzi pale Mtwara aliniambia huyo jamaa alikuwa ni miongoni mwa wachoraji wa Mr PUNCH alipokuwa Chuo Kikuu..
Huyo "mwanapunch", alikuwa mkimya, mwenye macho makali na maangavu. Anapotembea katika kundi la fungua zake mkononi, hupenda kuizungusha mojawapo katika ya vidole mithili ya anayetaka kuitumia kwenye kupekecha. Ukiingia ofisi kwake, kulikuwa na manira nyeupe juu ya meza nyeusi. Anapoketi, kwenye pembe ya mkono wake wa kushoto palikuwa na michoro midogo miwili. Mmoja ulikuwa kichwa cha mtu/nyani mwenye sikio kubwa kuliko kichwa chake. (Kwa maelezo hayo, wenye kumjua watamjua na kama humjui wewe furahia tu maelezo)
Hata hivyo leo ninanmaswali kadhaa ya kujiuliza ambayo sikuwahi kupatiwa majibu.
1. MR PUNCH alianza shughuli zake mwaka gani?
2. Nani walikuwa waanzilishi wa MR PUNCH? Ikiwa unafahamu madhumuni yao, si vibaya kutuambia.
3. Usajili, recruitment, wa wanapunch ulikuwa unafanyika ki namna gani?
4. MR PUNCH lilikuwa ni neno la siri (coded word) ambalo kifupi chake ndiyo ikawa hivyo au lilikuwa hivyo hivyo.
5. Kwanini walitumia jina lenye jinsi ya kiume na nyakati fulani kuhusishwa na kuwanyanyasa wanawake pale chuoni?
6. Katika jamii inayoishi, ni kweli MR PUNCH imekufa au ni kwamba iko dormant?
Tafadhali karibu kwa mchango wako.