Mr. Blue na Baki na Mimi

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Asalam alaykum wanajamvi...
Mimi ni mpenzi wa nyimbo za kuchana au kupasuka kama wengi wasemavyo, kinachonifanya nisipende nyimbo za wabana pua sababu kubwa ni
1) Kuigana
2) Point kuu Mapenzi
3) Taarabu yaani mipasho
Katika nyimbo nyingi hazina maudhui ya maana zaidi ya Mapenzi tu huyu kamsifia demu wake na yule kamsifia bwana ake.
Wengine wanaimba mipasho yaani ugomvi wao mtaani wanauleta kwetu kwa njia ya nyimbo, huyu kamtukana yule na yule kamtukana huyu kumjibu.
Wengine swagger hawana hivyo wanaiga kuanzia namna msanii fulani anavyoimba mpaka aina ya maudhui ya nyimbo zao. Mfano asilimia kubwa ya wasanii wa sasa wanamuiga Diamond Platinumz kuanzia uimbaji, uvaaji, uongeaji, uchezaji, skendo n.k in short hawana ubunifu wa maana.
Katika wasanii ambao sijawahi kuona kachuja au kuiga style ya mtu basi Mr Blue anahusika sana. Huyu jamaa tangu anatoka akiwa kijana mdogo mpaka sasa ana zaidi ya miaka 12 katika fani yake. Nyimbo zake nyingi sana nazikubali kuanzia swagger zake binafsi, uimbaji wake, dhima ya nyimbo zake ni msanii unique ambae amebaki kwenye game kwa muda mrefu sana.
Hili ngoma lake la Baki na Mimi nimelielewa sana kuanzia kwenye beat yaani daah, namna alivyoflow ndani, mitupio yaani swagger zake mdogo mdogo lakini hakuna msanii kama huyu...wasanii Wengine ambao hawajawahi kuniangusha ni
-Fid Q
-Joh Makini
-Ambwene Yesaya
-Mwana FA
-Professor Jay
Ni baadhi ya wasanii ambao nakubali sana kazi zao..Ila kwa nyimbo ya BAKI NA MIMI aisee Mr Blue big up sana...!!
 
"Mbona Ney wa mitego naye anaimba Taarabu kwa beat za hip hop mfano... Dj choka daily bata hivi huna familia??????????????????"
Ndio maana nikawataja wasanii ambao hawajawahi kuniangusha, kuipenda mingoma ya kupasuka haimainishi napenda nyimbo zote za kupasuka la hasha...
Fid Q ndio msanii pekee wa Hip Hop ninayemkubali na ngoma zake zoooote yaani hakuna hata ngoma yake moja nisiyoikubali, huyu jamaa kabarikiwa aiseeeeee
 
Nyimbo nyengine akiimba msanii asiyejulikana itaonekana makelele tu,mfano kama hiyo nyimbo ya Blue yani anatukana tu hakuna kitu.
 
Msanii ambaye yuko unique ni Shilole peke yake. Mr. Blue anaimba nini bitoz tu.
 
Ndio maana nikawataja wasanii ambao hawajawahi kuniangusha, kuipenda mingoma ya kupasuka haimainishi napenda nyimbo zote za kupasuka la hasha...
Fid Q ndio msanii pekee wa Hip Hop ninayemkubali na ngoma zake zoooote yaani hakuna hata ngoma yake moja nisiyoikubali, huyu jamaa kabarikiwa aiseeeeee
Na usipokuwa timamu kichwani kumwelewa ngosha ni mkali ni ngumu sana!kiukwel anajua pia ni my no1 hphp star in Tz....
 
Fid anajua sana, tatizo hajui kufreestyle...ndo maana nimeamua kumkubali MBISHI badala ya fid.
 
Ni kweli matusi sikatai angeimba mwingine isingesikika sababu Blue ana swagger zake zilizopelekea nyimbo ibambe...
Kiukweli ile nyimbo kwa mimi ni nyimbo ambayo ni chini ya kiwango kwa Blue,ila ukishakuwa msanii mkubwa watu huwa wanajaribu kukuelewa ni tofauti na msanii wa kawaida tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom