Mpuuzeni Mkuchika,hajuwi alisemalo: Prof.Lipumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpuuzeni Mkuchika,hajuwi alisemalo: Prof.Lipumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Oct 5, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka Watanzania kumpuuza naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, George Huruma Mkuchika kwa madai kuwa hajui anachokifanya.

  Mkuchika alisema wakati akihutubia sherehe za Umoja wa Wanawake wa CCM kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kwamba suala serikali ya mseto visiwani Zanzibar halipo.

  Kauli yake imepokewa kwa hisia kali na viongozi wa juu wa CUF wakati walipozungumza na Mwananchi jana, wakisema waziri huyo wa nyumba na maendeleo ya makazi anatoa kauli zinazopingana na kauli za viongozi wake wa juu.

  Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alisema Mkuchika ana tatizo la kumbukumbu ya mazungumzo mbalimbali ya muafaka baina ya chama hicho na CCM tangu mwaka 2009.

  “Mkuchika hajuia anachokifanya kwa sababu suala la serikali ya mseto limesemwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, makamo mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa, Samuel Malecela na Kingunge Ngombale Mwiru,” alisema Profesa Lipumba.

  “Hivi msemaji wa CCM ni nani hasa mana hawaeleweki kila mmoja anasema lake; kauli zao zinapingana; wapowapo tu hawaeleweki hata kidogo. Mimi nashindwa kuielewa CCM, naona inajikoroga tu”.

  Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohammed alisema wameingia katika mazungumzo na CCM mara kadhaa tangu mwaka 1999, lakini wamekuwa wakikwepa.

  “Baba wa Taifa alishasema kwamba suluhisho la mpasuko wa kisiasa Zanzibar ni serikali ya mseto tu, sasa leo Mkuchika anakuja na kuanza kutoa kauli zinazopingana na viongozi wake eti kwa madai serikali ni yao,” alisema Mohammed.

  Alisema katika mwafaka wa 1999 kila ajenda na kipengele kilichokuwa kinajadiliwa kilikuwa kinatiwa saini na Omar Ramadhan Mapuri kwa upande wa CCM na Abubakar Khamis kwa upande wa CUF na ilipofika mahali pazuri CCM wakapiga chenga.

  “Katika mwafaka wa 2005 kila ajenda tukatiliana saini, kikabakia kipengele cha mwisho... kilichobaki ni utekelezaji. Wenzetu kama kawaida yao wakaja na hoja ya kura za maoni.

  Halafu katika nyaraka yao kwenda NEC tunayo inasema hoja hiyo ni kuipiku CUF kisiasa tu,” alisema Mohammed.

  Alifafanua kuwa walitiliana saini na CCM kwamba kila chama kinachopata asilimia 30 ya kura katika uchaguzi wa rais lazima kishirikishwe katika uundaji wa serikali na kwamba ushahidi upo.

  “Sasa Mkuchika anaropoka tu lakini hajui na hana kumbukumbu ya kile anachokizungumza kwa wenzake wamesema nini,” alisema Mohammed ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Wawi kisiwani Pemba (CUF).  Source: Mwananchi
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Natamani Mkuchukika angekuwa ni mkaazi wa Zanzibar asingelisema pumba zake
   
Loading...