Mpito wa kisiasa

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
842
512
Katika zama hizi za mpito wa kisiasa baada ya kuondokewa na rais wa nchi yetu kumejitokeza mambo mengi, lakini kwa leo nataka nijikite kwenye hili la KUFA KUFAANA. Tumeona na kusikia watendaji wengi serikalini wakichukulia hali hii kama fursa ya kupata kipato isivyo halali.

Polisi wa Babati baadhi yao nao hawapo nyuma katika hili, hasa oc cid. Amekuwa akitumia muda huu kuwarundika mahabusu raia pasipo kutoa mdhamana. Ili kupata mdhamana lazima utoe fedha kwanza.

Kuna watuhumiwa wa wizi wa n'gombe wapo ndani tangu tarehe 19 machi na hadi leo hii hawakuwa na mashitaka ya kueleweka wanayotuhumiwa nayo. Katika kipindi chote hiki amekua akidai dau kubwa la fedha toka kwa ndugu za watuhumiwa. Alipoambiwa awafikishe mahakamani alidai jalada lipo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Ndugu walipofuatilia walibaini hakuna jalada lililopelekwa. Habari za uhakika toka kwa askari waadilifu ni kwamba ameamua kuwaandikia mashitaka ya kutakatisha fedha ili wasipate mdhamana na kuwakomoa kwa kukataa kumhonga.

Takukuru mkoa wa Manyara wachunguze hili kwa kuangalia hali halisi katika kituo hiki cha polisi.

Watendaji wa aina hii ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa letu.
 
Uzeen wanaishigi maisha ya shida sana polic wa aina hii.

Kuna mmoja morogoro kakaa kwenye nyumba ya serkali hadi kaondolewa kwangu.

Yaan kastafu lakini.alipigika hadi.kakosa hata pakwenda.

Police wanapenda sana pesa chafu ambazo ndio zinawafanya waishi kwashida uzeeni.
 
Back
Top Bottom