Wordsworth
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,177
- 3,316
Jamani jamani kati ya vitu tulivyorithi kutoka kwa wakoloni wetu hawa wa mwisho ni majigambo!
Mpira wetu na wao unafanana kwa kuchezwa na mdomo. Tena bora hata wao wanajitahidi timu yao ya taifa hata inafuzu kwenye michuano ya bara lao na ya dunia. Sisi sasa, hata kufuzu ya Afrika tu imekuwa ni ndoto. Yaani mpira ungekuwa maneno aiseee tungeongoza Afrika. Yaani tungekuwa tunafukuzana na Brazil kwa mataji ya World cup! Lol
Tulikaribia kufuzu CAF ila sasa tulivyojisifu utafikiri tumeshinda kombe la dunia. Utasikia mara ooo kikosi chetu ni bora, nilimsikia mchambuzi mmoja akidiriki kusema kwa mwaka 2018 kikosi chetu ni kati ya vikosi bora Africa, wakati hata East Africa tu tupo mkiani. Ingetokea muujiza tu taifa stars wakafika robo finali CAF aiseee nchi nyingine za bara hili wangetafuta bara lao. Manake siyo kwa hayo majidai.
Ukija kwenye club ndo majanga! Hasa hasa Simba na Yanga. Tena bora hata Yanga, Simba sasa ukimchanganyia msemaji wao Haji Manara na endorsements mbali mbali za maceleb utajua bonge moja la klabu yaani kama vile Real Madrid. Utasikia wakisema mfalme wa nyika hua nachekaga mwenyewe. Mpira ungekuwa maneno aiseee Tp Mazembe wasingeona ndani kwa wekundu wa msimbazi. Lakini bora hata Simba leo imeshinda waendelee kuwakilisha taifa japo ni kwa tabu sana.
Kwa majigambo na maneno tupo vizuri aisee. Wangeanzisha tu kombe la dunia la kujitamba tusingeshindwa kamwe labda ushindani wetu ungekuwa Uingereza tu. 😂😂 Yaani huwa nikiwaza mwenywe nacheka na kufurahi kuzaliwa Mtanzania, na shuhudia mubashara kabisa maajabu ya ulimwengu huu.
Na hii sio mpirani tu hata sekta nyingine za nchi Watanzania jamani tunaongea! Ni bora tungechukua hatua zaidi katika kuboresha mpira na michezo mingine kuliko kuzungumza sana. Bora tujigambe tukiwa na cha kujigambia.