myao wa tunduru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2010
- 615
- 234
Kama kuna mdau yeyote wa soka aliyebahatika kumsikia huyu jamaa katika kipindi cha mchezo redio Clouds bila shaka atakubaliana nami kama jamaa ana kipaji cha kuongea na kama mpira ungekuwa unachezwa mdomoni basi huyu jamaa kiwango chake tungefananisha na kina Messi!
Ningependa tupeane baadhi ya maneno yake anayoyatumia!
Anakuambia yeye fundi wa mpira ukiutaka mpira anakupa kama hataki anakufanyia ubahiri anapiga nje ya kumi na nane mabeki wakizubaa anawafanya kama mahindi machanga hatemi kitu anayatafuna gudugudu!
Huyo ndo Mbwiga baba na mama yake Wazaramo yaani kama sketi na blauzi. Usafiri wa kwenda kijijini kwao uzaramoni anapandia Buguruni stendi siyo Ubungo Bus Terminal!