Mpira ungekuwa unachezwa mdomoni, Mbwiga Mbwiguke wa Clouds FM angekuwa na kiwango cha Messi!

myao wa tunduru

JF-Expert Member
Mar 9, 2010
615
232
Kama kuna mdau yeyote wa soka aliyebahatika kumsikia huyu jamaa katika kipindi cha mchezo redio Clouds bila shaka atakubaliana nami kama jamaa ana kipaji cha kuongea na kama mpira ungekuwa unachezwa mdomoni basi huyu jamaa kiwango chake tungefananisha na kina Messi!

Ningependa tupeane baadhi ya maneno yake anayoyatumia!

Anakuambia yeye fundi wa mpira ukiutaka mpira anakupa kama hataki anakufanyia ubahiri anapiga nje ya kumi na nane mabeki wakizubaa anawafanya kama mahindi machanga hatemi kitu anayatafuna gudugudu!

Huyo ndo Mbwiga baba na mama yake Wazaramo yaani kama sketi na blauzi. Usafiri wa kwenda kijijini kwao uzaramoni anapandia Buguruni stendi siyo Ubungo Bus Terminal!
 

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,548
Jamaa aliizungumzia mechi ya Simba na Mfulila Wonderers 'spelling sina uhakika' nikawa kama naiona mechi. Simba alipigwa nne mtungi nyumbani na yeye ugenini akapiga mtu tano kibuyu. Jamaa ni noma.
 

Kesban

Member
Mar 26, 2009
13
7
Mbwiga ana maneno sana, anakwambia ....sio kubadilikabadilika km sauti ya muuza samaki, akiwa mtaani anauza samaki anabana pua, akirudi nyumbani sauti kibesi, teh!
 

Kesban

Member
Mar 26, 2009
13
7
'Anakwambia nr 9 uwanjani anatakiwa awe km gobagoba(I'm not sure)' yaani huko hilo pikipiki sio pikipiki, gari si gari, in short inafanya shughuli zote.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,443
jamaa anaujua mpira ule wa kwetu enzi zile tunaruka ukuta tunatua mzunguko halafu unajimwagia maji uanawapa manesi wa red cross mia tatu wanakuvusha kukunawisha unapotelea green stand

tamu sana hizi simulizi

kijiwe
 

myao wa tunduru

JF-Expert Member
Mar 9, 2010
615
232
Msikilizeni Mbwiga. Nimejaribu kuupload one of the few recordings za mbwiga, I hope itawork. Au mnielekeze ntaziwekaje humu ili nanyi mfaidi.

mkuu imekubali plz endelea kutupia!huyu jamaa namkubali sana hapo nimeisikiliza.....burudaaaniiii!huyu jamaa ana kipaji cha kuongea
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,858
10,362
Namsubiiri leo saa 3 hii ili nimsikie baada mechi ya watani na ukizingatia yeye mbwiga ni mshabiki mkubwa wa simba s c
 

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,102
126,470
kama kuna mdau yeyote wa soka aliyebahatika kumsikia huyu jamaa katika kipindi cha mchezo redio clouds bila shaka atakubaliana nami kama jamaa ana kipaji cha kuongea na kama mpira ungekuwa unachezwa mdomoni basi huyu jamaa kiwango chake tungefananisha na kina messi!ningependa tupeane baadhi ya maneno yake anayoyatumia!...........anakuambia yeye fundi wa mpira ukiutaka mpira anakupa kama hataki anakufanyia ubahiri anapiga nje ya kumi na nane mabeki wakizubaa anawafanya kama mahindi machanga hatemi kitu anayatafuna gudugudu!huyo ndo mbwiga baba na mama yake wazaramo yaani kama sketi na blauzi usafiri wa kwenda kijijini kwao uzaramoni anapandia buguruni stendi siyo ubungo bus terminal!

naomba cv yake fasta
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

8 Reactions
Reply
Top Bottom