Mpira- Soccer- Football- Kabumbu

Mario Kejob

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
441
536
Kumekuwa na ongezeko kubwa la ushabiki katika mchezo huu pendwa katika Tanzania na kupelelekea kusajiliwa kwa wachezaji wengi kutoka nje. Hii imesababishwa kwa kukuwa kwa nguvu za kiuchumi na kuifanya ligi hii kuwa ni kimbilio la wachezaji katika ukanda huu.

Yapo mambo ya kimsingi ambayo bado tuna lag behind ikiwa ni pamoja na viwanja bora vya mchezo huo.

Viwanja vingi vya mikoani bado vipo katika hali duni sana na hivyo kuwaomba wahusika wafanye jitihada kwani ligi sasa inapanuka na kuangaliwa na watu wengi wakiwemo wa nchi jirani kupitia kwenye tv na social media.

Wangejihidi walau viwanja hivyo kuwa na nyasi bandia kwani ukiwaangalia Simba wakicheza uwanja wa Taifa ni tofauti kabisa na Simba ikicheza viwanja kama Mkwakwani. Kwa hiyo utakuta kuwa kiwango cha uchezaji kinategemea sana na hali ya uwanja unaochezewa mchezo huo.

Hivyo basi, tunawaomba wahusika waboreshe viwanja hivi na si vya ligi kuu tu na hata daraja la kwanza kwani mpira sasa hivi ni ajira kubwa na inayolipa. Kwa upande wa utangazaji hatuko vibaya na hapa napenda kuwapongeza Azam Tv kwa hicho wanachokifanya kulingana na uwezo wao.

Tunataka kina Samata kama hamsini hivi ili waweze kurudisha pato lao nchini na kuchangia maendeleo ya uchumi wetu. Yapo mengi yanatakiwa kufanywa and that's for another day.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom