kwa kuanza we nishabiki wa timu gani?!
Nashabikia / Supporter wa Timu ya mtaani kwangu haijapanda daraja lolote..., ila mimi ni muumini wa Mpira ninaangalia mipira yote na hufanya hivyo ili kuburudika.., na nikiona Timu ya Kitaa inadefend tu bila ku-attack hata kama wakishinda sifurahishwi na kile wanachokifanya
Ni kipi cha muhimu sana kwa washabiki ?, Je is football game of results ? au ni bora hata tukifungwa ila chenga twawala ?
Ni maneno mengi yamesemwa hata The GodFather of Boring (Jose Maurinho) alisema kwamba Westham inacheza 19th Century Football !!! ila tukiangalia ile Chelsea iliyoshinda ile Champions League kwakweli ilikuwa a sad day in football..
Swali langu ni kwamba Timu haina wajibu wa kuhakikisha kwanza inaburudisha ? Nina uhakika bila Brazil, Barcelona and Arsenals of this world..., mpira usingekuwa unaitwa the Beautiful Game...., Mpira ambao ni Negative utakupeleka so far ila baada ya kushinda Kombe hata mwaka mmoja mashabiki watachoka na kudai zaidi.., na ukiendelea hivyo unaweza kujikuta watu wanaacha kuangalia..For the good of Football ni bora mashabiki wakakemea hii cancer ya kupaki mabasi (Turudi kwenye Imani ya Kwamba Attack is the Best Defense)
it's your faith.. you should not force me to just believe what you say...
my question to you..why say it now?
Njoo kule CHELSEA FC THREAD lete hii hoja kule..si umemtaja CHELSEA FC 'coach', njoo kule..tuongee vizuri.🙂
Nashabikia / Supporter wa Timu ya mtaani kwangu haijapanda daraja lolote..., ila mimi ni muumini wa Mpira ninaangalia mipira yote na hufanya hivyo ili kuburudika.., na nikiona Timu ya Kitaa inadefend tu bila ku-attack hata kama wakishinda sifurahishwi na kile wanachokifanya
sasa kama unashabikia timu ya mtaani kwenu, morinho hapo ameingiaje?! .......... uliangalia game la atletico vs barcelona?!
Hapa hakuna unafiki ndio maana nikataja maneno aliyosema Jose mwenyewe kuhusu West Ham kwamba wanacheza 19th Century Football au msemo wa kupaki basi aliuleta Jose mwenyewe siku walivyocheza na Spurs wakatoa draw akasema kule Ureno hii huwa tunaita kwamba Timu inakuja na basi lao wanalipaki golini..., sasa na mimi kama Neutral nikiangalia soka lao je nakatazwa nikisema Jose ni Godfather of Boring ?we tatizo lako thread yako imekaa kinafik nafiki zaid!" ungeanzisha bila kutaja chels cjui wamapaki basi final, ndio mana nikauliza gemu la atletico vs barcelona uliangalia?! uliona atletico walivyocheza?! siyo unashupalia chels chels!" 2achane na hay0 ........... nikuulize swali jingine " je unafikiri ni kw nn Moyes amefukuzwa?" na timu ilikua inacheza vizur hata hao chels hawaoni ndani.
sasa kutakuwana ladha gani endepo timu zote zitacheza mpira wa aina moja? hao aseno unaowasifia kwa soka safi mbona washabiki wake bado wana malalamiko ya kutaka vikombe? kilka timu ina falsafa yake katika soka
I say it now because there is a tendency of results by all means.., na ni ukweli usiopingika kwamba haina hii ya negativity itafanya watu wasipende mpira.., kuna sababu kwanini Italian Football haiangaliwi sana (defensive) na kuna sababu Timu kama Ajax, Barcelona, Real Madrid zinapendwa hata na Neutrals.., Ni ukweli usiopingika kwamba Negativity in the long run inaua mpira na kupoteza mashabiki..
Ndio unaweza ukashinda Makombe kwa kuwa Negative (Hata Greece ilishinda Kombe la Ulaya) lakini kila mtu akitumia hii negativity (sio kwamba hawawezi) watu wataacha kuangalia mpira..
Kwanza nakushauri ungebadili heading ya uzi wako.
Ukimaliza, jaribu kutupa definition/maana ya negative football na ukiweza mbadala wa hiyo negative football
Una vigezo vipi kusema Italian football haiangaliwi sana (defensive)?
Haiangaliwi na nani na wapi?
Sasa hapa uninilisha maneno, nimesema Timu kama Ajax zinapendwa hata na Neutrals nikimaanisha aina ya mpira wanayocheza.., ukiachana na hii Ajax ya sasa kuna Ajax ambayo watu walikuwa wanasema ndio walioleta Total Football, pia sijasema AC Milan ni boring (the best Team of so many years, mfano ya Kina Gullit, Weah n.k.) au Juventus bali nimesema mpira wa Italy ni defensive as a whole sio AC Milan wala Juventus as a Unit.., ingawa Premier League ina Pace lakini bado kuna Teams za kina Sam zinazocheza Route One FootballUnaweza ukaweka data hapa kwa Ajax inapendwa sana kuliko AC Milan au Juventus?
Halafu wewe ni nani au unakibali gani kuwasemea watu kuwa "na ni ukweli usiopingika kwamba haina hii ya negativity itafanya watu wasipende mpira"?
Unapata wapi huu ujasiri wa kuwasemea watu hata usiowajua?
Sisemi kila timu icheze mpira wa aina moja bali timu zikiwa attacking minded mpira unavutia zaidi.., hivi unajua kwamba zamani mpira ulikuwa na points 2 draw point 1 na ukishinda points 2; hadi kuweka point 3 timu ikishinda ilikuwa ni ili kushawishi timu kuwa na mashambulizi.
Pia hivi unajua Arsenal kabla ya Wenger ilikuwa inaitwa Boring Boring Arsenal ? au One Nil to the Gunners ?, Hii ilikuwa sababu jamaa wakikufunga moja wanadefend mpaka mwisho na kwa taarifa yako Arsenal then ilikuwa haipendwi kama leo na washabiki hawakuwa wengi kama leo.., Pia timu kama Brazil ndio zimekuwa kama mabalozi wa kutangaza soka na kufanywa ipendwe kama inavyopendwa sasa.
Ndio maana hapa sijasema upende aina fulani ya Timu bali nimekuuliza, je Timu ikiwa effective inashinda na inashinda kwa winning Ugly, je inatosha ? au ina wajibu zaidi ya kushinda ?