Mpinzani mpya wa A. Mrema jimbo la Vunjo

Mpinzani mpya wa A. Mrema jimbo la Vunjo

MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Posts
712
Reaction score
332
Habari kwenu wanasiasa wote katika jukwa hili

Habari mpya ni kuwa amejitokeza kijana machachari ambaye anaonekana kukubalika na wengi. Huyu ni mtaalamu wa uchumi wa Jamii na amekua akifanya kazi na mashirika mengi ndani ya Mkoa wa KILIMANJARO.

kIJANA HUYU anaonekana kukubalika sana na makundi ya wanawake na vijana ambao Mh. huwa anayategemea sana. Kijana huyu anakubalika kwani kulingana na kazi yake ameweza kushawishi wengi katika shughluli za kiujasiriamali na hamasa kwa jamii ndi ya kata 15 za jimbo la Vunjo.

Kwa kujiamini kijana huyu toka familia ya aliyekuwa Mangi wa Kirua Vunjo aitwaye Mangi Mashingia amesema kuwa kupitia CHADEMA mambo na mahitaji muhimu ya watu wa Vunjo yatatekelezeka kwa kuweka mtandao mbadala katika kuleta maendeleo endelevu na sio kujisifia kama afanyavyo Mzee Mrema.

Yetu macho na masikio.
 
Bila shaka ni yule Kamanda Reg Mashingia....!! Kama ni yeye! ANAAMINIKA...ATAIWEZA VYEMA JIMBO KUBWA LA VUNJO! Ni mfano wa LEMA na jimbo la Arusha Mjini! Mashingia anaweza, anao vijana wasomi na wananchi wa Kawaida ambao watakuwa wanamuunga sana mkono ili kulinusuru jimbo hilo linalokalia Utajiri mkubwa wa Utalii kwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, kupitia route ya KINAPA Marangu, na pia anaweza kusimamia 'route' nyingine ya Utalii kupitia 'Kirua Makundishi' ambayo imejaa vivutio na vyanzo vya maji ya asili..!

PAMOJA DAIMA...!

Hakuna asiyejua kuwa Augustine Mrema ameshindwa kila kitu na imebakia tu kutoa majigambo! AONDOKE...amerithi kuwa 'mzigo' kama CCM wanaomfadhili mafao.
 
Mrema anategemea kusaidiwa na ccm,ndio maana haachi kumsifu JK
 
anaogopa mpaka kutaja au kutajwa jina si kashashindwa kabla hajaanza
 
Jimbo la vunjo tuna mgogoro na mkuu wa mkoa.kipimo cha mgombea 2015 ni kijana atakaye jitosa kuhakikisha wazazi wetu hawataporwa mashamba ya lokolova.vikao vya wana mwika kusini vinaendelea.mbunge aliyepo kashachukua rushwa 200mil vielelezo vipo muda ukifika tutaweka kila kitu hapa.
 
Back
Top Bottom