Mpinzani kwa kweli wa ccm ni serikali yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpinzani kwa kweli wa ccm ni serikali yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chegreyson, Dec 8, 2011.

 1. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 735
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Leo nimeona nianze kuchokoza mada ya hapo juu kuweza kujua matatizo ya nchi yetu,hasa katika awamu hii ya nne ambayo maamuzi mengi ya msingi hayafanywi au yanaachwa yafe kifo cha mende.
  Nionavyo mimi CCM imeuza kukubalika kwake kwa wananchi kutokana na serikali yake kutotekeleza malengo waliyopangiana na wakati huohuo kufuja mali ya wanyonge bila huruma,kuwa na viongozi wanaotoa siri za serikali upinzani na kwa makusudi kuacha kufanya kazi za taalum zao na kujiingiza katika ushabiki wa kupindukia wa kisiasa.Kansa hii ni ya hatari kwa maana hata upinzani wakichukuwa nchi bado civil service itawatafanya black mailing kwa watawala wapya in the process kuzorotesha maendeleo ya nchi na watu wake kwa ujumla
  CCM leo hawana hata mtu mmoja ambaye anaweza kusimama kidete na kuwakemea wenzake kuwa njia wanayopita sio sahihi na wamekosea hivyo wanapaswa kubadilika na kusoma alama za nyakati .Kama ilivyokuwa wakati wa Mwl ambapo alikuwa na uwezo wa kukemea wakamsilikiza.
  Hiyo power vacuum iliyopo ndiyo tiketi ya CDM kushika nchi.
  Sio kwamba cdm ni wazuri ki vile la hasha ila kwa kadri mambo ndani ya serikali na ccm yanavyokwenda, watu wamekata tamaa na kutafuta mbadala.
  Ndio maana leo hii wakati halmashauri kuu ya ccm inapokaa kila kinachojadiliwa ndani kinatoka nje live na wao wenyewe wanashangaa.
  Kwangu mimi swala la kujivua gamba lingeamliwa hivi.
  "Bwana Lowasa,Rostam,Chenge,tunawapendeni kama wenzetu,lakini kwa kuwa MACHONI PA WATANZANIA HAMTAZAMIKI CHAMA KINAWAVUA NYAZIFA ZENU ZOTE NA KUWAFUTA UANACHAMA".
  Baada ya uamuzi huo mngeenda chini kwa kila tawi,na kujisafisha .
  Kwa kufanya hivyo mngeheshimika na labda watu wangeanza kuwa na inani kidogo na ccm
  Swala jingine safu yenu ya uongozi haina haiba ya mvuto unaotakiwa .

  Bila kutafuna neno Mukama,Msekwa,Chiligati,hawana mvuto kwa namna ye yote ile,hivyo kuwagarimu sana.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo titlle tu nakupa 0% ya kufikiri
   
Loading...