Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Luhaga Mpina, aliyekuwa mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, leo Oktoba 27, amezungumzia rufaa yake aliyokata katika Mahakama ya Rufaa baada ya Agosti 6, 2025, kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa JTM.
Septemba 13, 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea fomu zangu za uteuzi na kuniteua kuwa mgombea wa urais wa JMT kupitia ACT baada ya amri Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma Septemba 11, 2025.
Agosti 26, 2025, saa 11 jioni, Msajili wa Vyama alibatilisha maamuzi ya Mkutano Mkuu wa ACT ya kuniteua kuwa mgombea urais. Siku hiyo hiyo, saa 5 usiku, INEC ilinizuia kurudisha fomu kesho yake, tarehe 27 Agosti 2025, ambayo ilikuwa siku ya uteuzi wa wagombea wote wa nafasi ya urais wa JTM.
Uamuzi wa kunizuia kurudisha fomu ulitupiliwa mbali na Mahakama Kuu ya Tanzania, ambayo pia iliagiza INEC ipokee fomu zangu na kunirejesha katika mchakato wa uteuzi. Baada ya kurejesha fomu Septemba 13, 2025, niliwekewa pingamizi tatu.
Moja ya pingamizi hizo liliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari. Kwa maoni yangu, aliyeniwekea pingamizi hili ni mgombea urais kupitia CCM, ndugu Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea urais wa vyama vya NRA na AAFP.
Inashangaza wagombea urais watatu kuniwekea pingamizi baada ya kuteuliwa na fomu zangu kuwekwa kwenye ubao wa matangazo wa INEC, lakini wakati wagombea wenzangu 17 wanateuliwa, hakuna aliyewekewa pingamizi hata mmoja. Kwanini Mpina? Kwa kosa gani? Na kwa manufaa gani? Ni manufaa kwa taifa au binafsi?.
Nachukulia kwa uzito mkubwa taarifa aliyoitoa hivi karibuni mwanasiasa mkongwe na mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini, Selemani Saidi Bungara, kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa amekuwa akitumika kutengeneza migogoro ndani ya vyama vya upinzani ili kudhoofisha nguvu ya demokrasia na upinzani nchini.
Kitendo cha Msajili wa Vyama kuingilia mchakato wa uchaguzi ndani ya vyama vya upinzani na kujigeuza kuwa mtoa maamuzi na hukumu bila kujali utaratibu uliowekwa kikatiba, kikanuni na kwa miongozo katika kufikia maamuzi ya vyama, pamoja na kutengeneza taarifa za uongo na kuzifanyia kazi, ni mambo yanayoshangaza sana.
Kuanzia Oktoba 21 hadi 23, 2025 tulikuwa tumekamilisha adhima ya kukata rufaa kupinga kuenguliwa kugombea Urais katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu, Dodoma.
Nasisitiza kuwa ni muhimu sana uchaguzi wa nafasi ya Rais usifanyike hadi hapo Mahakama ya Rufaa itakapokuwa imetoa uamuzi juu ya rufaa yangu [kupinga kuenguliwa kugombea Urais].
Kilichonipeleka mahakamani si tu Mpina na ACT Wazalendo kurudishwa kwenye sanduku la kura kwenye nafasi ya urais, bali ni kupigania muktadha mwema wa vyama vya upinzani na kupata heshima inayostahili kwenye taifa.