Mpina kuwania uraisi kupitia ACT

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,039
Chama cha ACT Wazalendo kimependekeza majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kufuatia kikao kilichofanyika jana Jumanne, Agosti 5, 2025 katika makao makuu ya chama hicho, kwenye ukumbi wa Hakainde Hichilema.

Soma pia: Mpina agonga hodi ACT Wazalendo na yupo tayari kugombea urais



Katika taarifa iliyotolewa mapema leo asubuhi, Agosti 6, 2025, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho, Shangwe Ayo, majina yakiyopendekezwa kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Luhaga Mpina, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kisesa kupitia Chama Cha Mapinduzi, pamoja na Aaron Kalikawe.

Kwa upande wa Urais wa Zanzibar, jina la Othman Masoud Othman, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama na Makamu wa Kwanza wa Rais amependekezwa baada ya kuchukua fomu ya kuwania Urais peke yake.

Taarifa ya ACT Wazalendo imeeleza kuwa majina yote ya wagombea yatawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.

Aidha, Halmashauri Kuu ya chama hicho imeridhia uamuzi wa kiongozi wa chama hicho, Dorothy Jonas Semu, kujiondoa katika kinyangányiro cha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chanzo: Eatv
 
Bad move
 
Umoja, mshikamano, na uzalendo ndio nyanja kuu za maendeleo katika Taifa 🇹🇿 kwahiyo ndugu zangu tusibabaike wala kutangatanga msimamo wetu ndio maendeleo yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…