Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Katika mipasho ya Mama kwa Mpina, alidokeza kwamba wasimteue kugombea ubunge ili yeye amfikirie katika nafasi ya viti maalum vya Wabunge. Wenye akili tunatambua kuwa raisi alikuwa anamtafutia Mpina sehemu ya kumpasua, na Mpina akaingia kwenye kumi na nane zake. Huo mpasho haukuwa tukio la ghafla, ulikuwepo kichwani kilichokuwa kikitafutwa ni nafasi ya kuutoa.
Bila shaka Mpina anamheshimu Raisi kiasi kwamba hawezi kumjibu katika mpasho wake huu. Ila ndani ya moyo wa Mpina najua anajisemea kimya kimya kwamba, toka kuwa waziri, hivi raisi amenishusha mimi hadi kuniona mie ni mtu wa kupewa ubunge wa zawadi wa kiti maalum?
Unahitaji tu kuangalia aina ya watu wanaopewa ubunge wa viti maalum, iwe CCM au Chadema. Na wengine, hasa wanawake, tunajua walipewa kwa sababu walikubali kujitoa katika mambo ambayo sitaandika humu. Ndio maana utakuta wabunge wa viti maalum mara nyingi ni wanawake.Tunajua hilo, na hawa mara nyingi michango yao Bungeni ni pumba sana, yaani ni kelele za kishabiki na umbea tu, hakuna point ya maana wanayoongea Bungeni wakipewa nafasi.
Ndio, wapo wale wachache watapewa Ubunge wa viti maalum ili wateuliwe kuwa mawaziri. Lakini tunajua kuwa raisi hana mpango wa kumpa ubunge wa viti maalum Mpina ili amteue kuwa waziri. Mpina ni aina ya watu ambao ni wenye akili na kuona mbali ambao mtu yeyote mwenye uwezo huo mdogo hawezi kukubali awe nao karibu.
Hivyo Mpina ana jibu ndani ya moyo wake kwa raisi - ni afadhali nikalime pamba kuliko kukubali zawadi yako ya ubunge wa viti maalum, kwa kuwa eti nimeongelea mambo ya kitaifa wakati mimi ni mbunge wa jimbo.