MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, ameitaka serikali kuwarejeshea wenyeviti wa vitongoji mihuri yao iliyondolewa kwa madai yasiyo na msingi.
Akizungumza leo Aprili 23 bungeni jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mpina amesema hatua hiyo imepunguza mamlaka ya viongozi wa msingi wa serikali.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Sababu ya kuondolewa mihuri kwa wenyeviti wa vitongoji haina msingi. Kama hoja ni kuuza ardhi, basi hata watumishi wa wizara wanauza viwanja mara mbili, lakini hatujawahi kuwavua mamlaka yao,” amesema Mpina.
Amesisitiza kuwa mihuri ni nyenzo muhimu kwa viongozi hao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, hivyo Serikali inapaswa kuirejesha kwao ili waendelee kutoa huduma kwa ufanisi.