Tetesi: Mpina agonga hodi ACT Wazalendo na yupo tayari kugombea urais

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi...

Soma >> GE2025 - Luhaga Mpina ajiunga na ACT Wazalendo akitokea CCM
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimesoma habari hii nikaona niilete hapa Jukwaani kama ilivyo bila kuongeza neno wala kupunguza neno. Ila kama ni kweli basi nasema ya kuwa Amepotea njia na kujipoteza na atarejea CCM huku akiwa anabubujikwa machozi ya Majuto.

Hii hapa habari yenyewe 👉 Na Mwandishi Wetu

Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi, hadi kupelekea kusimamishwa kuhudhuria vikao kadhaa vya Bunge,” alisema Macheyeki.

Aliongeza kuwa, katika kipindi ambacho CCM haikubaliki na CHADEMA wakiwa wamefungwa minyororo ya uonevu, ACT-Wazalendo inatazamwa kama tumaini pekee lililobaki kwa wapiga kura, hivyo wanapaswa kuwa na mtu atakayeonekana machoni mwa wapiga kura kuwa tumaini lao.

“Mimi mara zote nimekuwa nikishauri chama kutafuta mgombea ambaye atakidhi kiu ya wapiga kura, mgombea ambaye ataziba pengo la CHADEMA kutoshiriki uchaguzi. Tunahitaji mgombea urais mwenye nguvu na ushawishi, mgombea ambaye anakubalika kwa wananchi na mwenye uwezo wa kuyaunganisha makundi yote ya wapiga kura,” alisema.

Kwa maoni yake, Macheyeki alisema kuwa kati ya wagombea waliotia nia ya urais kupitia ACT-Wazalendo bado wanakosa sifa hizo, na kwamba ni watu wasiojulikana maeneo mengi, hali itakayofanya kuwe na ugumu wa kuhamasisha wapiga kura waliokata tamaa, hasa kwa dhamira ya kupambana na dola.

“Chama hiki si mali ya Zitto, si mali ya Dorothy, si mali ya OMO, si mali ya Mchinjita, wala mali ya yeyote—ni mali ya wanachama wote. Na mtu yeyote ana haki ya kugombea. Sisi si CCM wa kutoa fomu moja. Hatuwezi kuruhusu viongozi wa chama waamue nani awe mgombea bila kuwasikiliza wanachama na wananchi.”

Alisema vijana watamuunga mkono Mpina bila hofu yoyote, pasipo kujali nani atachukia kwa misimamo yao.

Viongozi wa ACT-Wazalendo, kwa nyakati tofauti, walipotafutwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hizo za Mpina hawakuweza kupatikana.

Hata hivyo, tayari chama hicho kimetoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kitaifa Agosti 6 mwaka huu, mkutano utakaoteua majina ya wagombea urais kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mnabadili lini mgombea bwana chawa mana Pole Pole kawakaba wanakutuma wewe unakuja kubwabwaja kama umekatwa kichwa na Chai Jaba kapigwa jab leo ile inaitwa kelebu hatapanua kinywa tena mana hajui lolote kwenye huu mchezo
 
Naona mnajitekenya na kujichekesha wenyewe kama mazuzu.
 
Kuna muda naiwaza Sana ile principle ya "Divide and rule", huwenda Kuna namna katika hii nchi inatumiwa Sana na CCM Ili kuudhofisha nguvu ya upinzani (CHADEMA).
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimesoma habari hii nikaona niilete hapa Jukwaani kama ilivyo bila kuongeza neno wala kupunguza neno. Ila kama ni kweli basi nasema ya kuwa Amepotea njia na kujipoteza na atarejea CCM huku akiwa anabubujikwa machozi ya Majuto.

Hii hapa habari yenyewe 👉 Na Mwandishi Wetu

Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi, hadi kupelekea kusimamishwa kuhudhuria vikao kadhaa vya Bunge,” alisema Macheyeki.

Aliongeza kuwa, katika kipindi ambacho CCM haikubaliki na CHADEMA wakiwa wamefungwa minyororo ya uonevu, ACT-Wazalendo inatazamwa kama tumaini pekee lililobaki kwa wapiga kura, hivyo wanapaswa kuwa na mtu atakayeonekana machoni mwa wapiga kura kuwa tumaini lao.

“Mimi mara zote nimekuwa nikishauri chama kutafuta mgombea ambaye atakidhi kiu ya wapiga kura, mgombea ambaye ataziba pengo la CHADEMA kutoshiriki uchaguzi. Tunahitaji mgombea urais mwenye nguvu na ushawishi, mgombea ambaye anakubalika kwa wananchi na mwenye uwezo wa kuyaunganisha makundi yote ya wapiga kura,” alisema.

Kwa maoni yake, Macheyeki alisema kuwa kati ya wagombea waliotia nia ya urais kupitia ACT-Wazalendo bado wanakosa sifa hizo, na kwamba ni watu wasiojulikana maeneo mengi, hali itakayofanya kuwe na ugumu wa kuhamasisha wapiga kura waliokata tamaa, hasa kwa dhamira ya kupambana na dola.

“Chama hiki si mali ya Zitto, si mali ya Dorothy, si mali ya OMO, si mali ya Mchinjita, wala mali ya yeyote—ni mali ya wanachama wote. Na mtu yeyote ana haki ya kugombea. Sisi si CCM wa kutoa fomu moja. Hatuwezi kuruhusu viongozi wa chama waamue nani awe mgombea bila kuwasikiliza wanachama na wananchi.”

Alisema vijana watamuunga mkono Mpina bila hofu yoyote, pasipo kujali nani atachukia kwa misimamo yao.

Viongozi wa ACT-Wazalendo, kwa nyakati tofauti, walipotafutwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hizo za Mpina hawakuweza kupatikana.

Hata hivyo, tayari chama hicho kimetoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kitaifa Agosti 6 mwaka huu, mkutano utakaoteua majina ya wagombea urais kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Thibitisha taarifa yako
 
Iwapo ni kweli, itakuwa ni blunder ile ile ya cdm ya 2015 kwa Lowassa. Hata hivyo kwa ACT atakuwa ni mtaji mkubwa maana bado haina ushawishi mkubwa huku bara.
 
Lucas unaandikaga mada ndefu sana afu point ni 1/10
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom