Habari wanabodi.
Nahitaji mtu ambaye atanisaidia upimaji wa viwanja vyangu viwili mpaka hatua ya kupata hati miliki title deed.
Kiwanja cha kwanza kipo Bunju Beach, DSM, kina nyumba na nilikuwa nimeshaanza taratibu za upimaji mpaka nikafika hatua ya kupata beacon number, ila tatizo ni kwamba huyu jamaa anayenifanyia hii kazi longolongo zimekuwa nyingi na hili zoezi limekuwa refu sana.
Kiwanja cha pili kipo Boko, DSM. Hiki kiwanja sijaanza hatua zozote za upimaji lakini TP hipo.
Kwa yeyote anayeweza kufanya hii kazi, bila longolongo ani PM ili tuweze kufanya kazi. Asante.