chaUkucha
JF-Expert Member
- May 28, 2012
- 3,382
- 1,212
Jana mpenzi wangu kanipigia simu na kuniambia ameibiwa simu yake ya laki 8 nikamuuliza wapi akaniambia ameibiwa mjini nikampa pole alafu akaniambia nimpe laki 4 na yeye ana laki 4 akanunue simu nyingine nikamwambia njoo home uchukue,
Mida ya saa 12 :30 kashafika nikampa laki 4 akaondoka kwenda kwao huku nyuma Mimi nikavaa mkoti mrefu na maski nikakimbia nikaenda kumsubiria mbele kaja kafika kwenye kona moja hivi nikaona hapa hapa ndo pa kumalizia mchezo fasta bila kupoteza muda nikampiga kabali ya maana na kuchukua laki 8 yote nikatokomea zangu.
Kufika home tu akanipigia simu huku akiwa analia nikamuuliza kulikoni akaniambia amekabwa na kibaka na kunyang'anywa hela yote nikamwambia arudi nije nimpe nyingine akaja nikampa laki 4 yake na mimi nikabaki na ya kwangu alafu akaniomba nimsindikize hadi kwao anahofia kukabwa tena nikamwambia alale ataenda kesho.
Masuala ya kurudishana nyuma kimaendeleo sipendagi laki 8 yote ununulie simu wakati Mimi mwenyewe simu ya laki 1 yenyewe sijawai kununua.
Sipendagi ujinga mimi.