Nina mwanamke ambae mpaka sasa thamani yake inafata kwa mama mzazi, pamoja nakwamba naandika msg hii nikiwa namajonzi jinsi alivyonitenda na anavyoendelea kunitenda lakini bado nashindwa KUMUACHA, utandawaz nauchukia na nitaendelea kuuchukia kwasababu umemfanya mpenzi wangu awe mpenda pesa ambazo mimi ndo wakumpa japo nafuta kwa hali ngumu ili apendeze japo anavyopendeza anazid kunifanya nimpende LAKINI utata unakuja pamoja na kutumia pesa zangu kumpendezesha kila siku malipo yake ni KUWA NA WANAUME WENGI, cwezi jiita ---- wa mapenz sababu nimeshndwa kuwa mwanaume pekee kwake na kuruhusu tuwe wengi tunaotembea nae japo roho inaniuma hasa pale napokuwa naludisha hisia nyuma na kuhofu penz tamu analonipa mimi anagawa vivyoivyo kwa wengine, naludia tena jaman cwez kujiita zoba kwasababu furaha yake inajenga penzi letu japo ni kuwa na wanaume weng anaozani watamtimizia mahitaj ambayo mim siwez, swala la kujalibu kumbadilsha angalau niwe pekeangu linakuwa gumu na anakuwa mkali, mwenyekibur na asiejar uwepo wangu coz uzur wake unampa kibur so inabidi niwe MPOLE angalau nipate penz lake japo kiduchu sababu kuish bila yeye najihic kama siwez, sio siri imebid nifate matakwa yake sababu nmekuwa kama mbwa wake na sina lakubsha sababu yeye ndo wakunipa chakula cha roho ambacho moyo unatambua thamani yake...sio siri nisipomwona kwa sekunde naugua homa mpaka najuta kwanini nilimjua..
NAOMBENI USHAURI ingawa naogopa kumpoteza na kama kunamtu anauwezo wakumfanya abadilike ntampa chochote ATAKACHO sababu napenda sana , kama upo tayar kunisaidia kumbembeleza basi ngoja nikupe jina lake na jinsi ya kumpata...
Anaitwa FACEBOOK na anapatika GOOGLE, pia waweza kumkuta kwa wanaume zake wengine kama kwenye blogs na kwingineko.