Mpendazoe yuko wapi?

Aliibeep JF kwa kuweka nyuzi tatu per day! Feed back aliyoipata sidhani kama ana hamu na CCM tena!
 
Anauguza mkia
 
Kuna wale wakurugenzi 13 waliokacha uteuzi nadhani huyu mpendazoe atapata amekubali kukatwa mkia
 
mkuu, hujui kuwa siku hizi kuna ugonjwa mpya unaitwa tail-lessnessiasis? nasikia ni ugonjwa mbaya sana!
 
Yupo Facebook .anashambuliwa alafu nahisi yule mzee sio mzima aka chizi
 
Bahati mbaya sana JF sio sehemu ya mipasho kama ninavyotazama hali ilivyo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii. Ukiingia humu kwa ajili ya maarifa hutapotea kirahisi. Ni kwa vile kuna dalili ya kukomaa kwa njaa ndo maana wakati mwingine zimekuwepo lugha za kuomba misaada kwa namna yoyote. Kwa ujumla JF bado ni pazuri sana ukiyatumia mawazo yako kwa kizazi hiki kilichopo na kinachokuja lengo likiwa ni kuishi kwa furaha.
 
Anaishi kwa matumaini kwani katika zile teuzi za mwendo kasi kuna wengine wamezipotezea hivyo anasubiria third selection.
 
Kwa utawala huu ukiwa msaliti ndani ya ccm lazima ukae pembeni bila ya kupata ajira yeyote iwe ndani ya chama au serikali
 
Huyu Jamaa ilifika mahali alikuwa kero , maana kila atakalo lisikia kuhusu Serikali anakuja kulitetea au kulipongeza akidhani mkulu atamuona ampe "ulaji" lakini naona na jiwe likaamue limpuuze.

Ni rahisi sana kuondoka CCM ukaenda Upinzani ukaendelea kubaki na "umaarufu" wako ila ngumu sana Kuondoka Upinzani na kwenda CCM na ukaendelea kubaki na Umaarufu wako.

Huyu jamaa kaona harakati zake zinapuuzwa kaamua kukaa kimya tu.
 
Yupo tu anapambana na hali yake baada ya kuona alichokuwa anakipigania hakileti matokeo yenye athari chanya

kutetea ujinga kwa kutegemea uteuzi ni upumbavu wa hali ya juu sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…