Mpendazoe atoa sh mil. 15 kama dhamana kesi ya uchaguzi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe atoa sh mil. 15 kama dhamana kesi ya uchaguzi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  HATIMAYE aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Segerea (CHADEMA), Fred Mpendazoe, amelipa sh milioni 15 katika Idara ya Fedha ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam ikiwa ni dhamana ya kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo uliofanyika mwaka jana ambayo yalimtangaza Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (CCM), kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo.
  Mbali na Dk. Mahanga wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
  Katika madai yake mlalamikaji ambaye ni Mpendazoe anaitaka Mahakama Kuu itengue ushindi wa Dk. Mahanga kwa kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 hazikufuatwa.
  Wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, jana ndiye aliyekwenda idara hiyo ya fedha iliyoko ndani ya jengo la Mahakama ya Rufaa nchini kulipa kiasi hicho cha fedha na kuwaonyesha waandishi wa habari risiti ya malipo hayo.
  “Hii ndiyo risiti ya kiasi hicho cha fedha nilicholipa mahakamani kama dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mteja wangu ….na kwa kuwa tayari tumeishalipa baada ya kuupata uthibitisho wa malipo haya, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ndiye atapanga tarehe ya kesi ya mteja wangu kuanza kusikilizwa rasmi kwani taratibu zote za kisheria tumeishazikamilisha,” alisema wakili Peter Kibatala.
  Machi nane mwaka huu, Jaji Profesa Ibrahimu Juma, alitupilia mbali pingamizi la wakili Jerome Msemwa anayewatetea wadaiwa, la kutaka mahakama hiyo imzuie Mpendazoe asiruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha mahakamani kwa sababu muda wa kuwasilisha fedha hizo ulikuwa umeishapita.
  Jaji Ibrahimu alitupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa halikuwa limekidhi matakwa ya kisheria na badala yake akalikubali ombi la Mpendazoe kuweka mahakama kiasi hicho cha fedha kama dhamana.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Vizuri sana, naiman mambo yatakwenda vyema!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  mpendazoe anawaamini hawa mahakim?
   
 4. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  asee kwa kweli mpendazoe sisi tuko nyuma yako huyo jamaa makongoro mahanga aliiba kura kabisa watu walikamatwa na polisi na mihuli ya tume karatasi za kupigia kura ambazo tayari zilikuwa zimejazwa mshindi mungu atakusaidia mpendazoe ata wakisema uchaguzi urudiwe utashinda kwani ulishashinda kabla watu wa segerea walikuamini wewe na si huyo fisadi makongoro
   
 5. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mtu akikubali kutoa kiasi chote cha pesa kama hiyo, ujue ana uchungu kwa dhuruma aliyofanyiwa. Pengine huyu jamaa alidhurumiwa haki yake kweli na anaamini mahakama inaweza kumrejeshea haki hiyo kutokana na ushahidi alio nao. Kuna hatari kwa Mh Mahanga kuwa waziri wa kwanza kupoteza uwaziri na kuenguliwa ubunge mwaka huu.
   
 6. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa wakati mwingine mahakama ndio kimbilio,najua Mpendazoe atapata haki yake. Tunakushukuru prof. Ibrahim,kwa maamuzi yenye haki ndani yake. Tunakuombea ushindi ndugu Mpendazoe.
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuombe Mungu haki itendeke. Kila la heri Mpendazoe
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Tuwa makini jamani! Mimi ni mpenda demokrasia lakini kwa Mpendazoe mhm... Ogopeni sana watu wanaoweza kufanya lolote for the sake of ubunge. Nakumbuka huyu jamaa alivyohaha wakati wa kura za maoni, mixa kuhama vyama na kuhama majimbo ya uchaguzi. Simjui vizuri Mpendazoe, sina uhakika na perfomance yake akiwa CCM. Ifike wakati tukubali kuwa si kila anayekuja kwa flag ya CDM ana nia ya mabadiliko, ni zile milioni nyingi tu. Ifike kipindi CDM ikatae watu wa kabila hii. Tunayo nafasi ya kuchipua wanasiasa chipukizi wenye mtazamo chanya, kuliko hawa wazee ambao ni maoportunist kwa jina la CDM. Naomba kuwasilisha!
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ni kweli unachokiongea mkuu....ila huyu jamaa ndiye aliyeleta utamu wa siasa katika nchi yetu, na kuwaduwaza kwa KnockOut wana CCM kwani ndiye Mbunge pekee ambaye aliacha ubunge hata kabla hajamaliza muda wake na kuhamia CCJ,kama unakumbuka Mzee Mwanakijiji alimpaisha sana na CCJ yake ila badae kilipukutika kama jivu la sigara...then kazi ya kuhama-hama ndio ikaanzia hapo..sasa jiulize posho,marupurupu, na zile fedha zinazogawiwa kwa wabunge pindi bunge linapovunjwa huyu jamaa alizikosa!!!!Lazima awe na uchungu kwa hilo, isitoshe huku nako kaibiwa kura!!Inawezekana nyuma ya pazia ana siri kubwa ya kuchuma alichopoteza..!!anyway lets wait n c the drama!!!
   
 10. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hebu gonga hapa kidogo upate kumjua huyu jamaa japo kwa kifupi..
  www.wavuti.com/.../fred-mpendazoe-mb-aihama-ccm-na-kuhamia-ccj.html - Marekani -
   
 12. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Ndugu,

  Nakubaliana na wewe. Huyo jamaa anauchungu sana na haki yake kama walivyo CDM/Wananchi wengine kwa kuchakachuliwa kura za Dr. Slaa.

  Shida yangu moja tu! Bilashaka kunawanasheria wengi hapa JF. Kwanini kesi kama hii iwe na gharama kubwa kiasi hiki? Kuna maana gani kuweka pesa nyingi kiasi hicho kama dhamana! Hivi ni wangapi wanaweza kutoa kiasi hicho cha pesa kutetea haki zao za msingi ktk chaguzi zenye utata kama huu? Nina maana mtangaza matokeo (mkurungezi) anapoamua kutoa takwimu tofauti akiwa amelindwa na polisi na kumwambia aliye nyanganywa ushindi aende mahakamani wakijua mlalamikaji hawezi kiasi hicho cha pesa?

  Hivi kutoka na mwendelezo wa kesi za hivi karibuni na zinazoendelea- (Rushwa wakati wa uchaguzi; EPA cases; Zombe's case....) Do you still trust our judiciary systems?
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hii sheria inayohitaji dhamana ya sh 15m ni moja ya sheria mbaya ambazo zinatakiwa kufutwa. Tunaambiwa ni haki ya kila mtanzania anayejua kusoma na kuandika na aliyefikisha umri fulani kugombea ubunge, wakati huohuo tunaambiwa ni wale tu wenye uwezo wa kulipa mahakamani 15m ndio wanaweza kuwa wabunge. Kina Mpendazoe wenye uwezo na hiyo dhamana ni asilimia ngapi ya watanzania? Na ni aibu iliyoje kuwa Mpendazoe ni mmoja wa waliopitisha sheria hii mbovu! Shame on you wabunge wapumbavu.
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Zitarudi tu, Mahanga akipigwa chini!
   
 15. K

  Kaisikii Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  angezitumia kwa mambo yake mengine baada ya kukosa hata zile za malipo ya miaka tano akiwa mbunge na akiziingiza katika ngwe ya 2015,ni mawzo yangu tu hayo kwa mpenda zoe.
   
 16. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  Sawasawa Mdau,Nakubaliana na wewe katika kutokujua Dhamira halisi za Mpendazoe,its hard to tell that!!
  Lakini kwa Ushindi yeye ndiye aliyechaguliwa na sisi wakazi wa jimbo la Segerea kuwa Mbunge wetu!! Binafsi nilikuwa Wakala wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu uliyopita kata ya Kiwalani,Jimbo la Segerea!! Katika kata hii tu tulipofanya majumuisho ya kura za Mbunge na Diwani,Chadema ilishinda katika Ubunge na Udiwani yalipotoka matokeo ya NEC yakaonyesha kinyume chake!!
  Situation ilikuwa observed hiyo hiyo,chadema ilishinda katika kata zaidi ya 80%,Yet kwa Mabavu saa nane Usiku kwa Mtutu wa Bunduki pale Anataglou MAHANGA akatangazwa mshindi!!
  In a nutshell,MPENDAZOE NDIYE MSHINDI,MAHAKAMA ISIPOMUOGOPA JAKAYA WATAMPA UBUNGE ALIYECHAGULIWA!!!!
   
 17. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kaka fred ukikaa kimya wananchi wataamini umehongwa. Mnaosema hizo fedha angezitumia kwa mambo mengine huo ni ubinafsi msifikiri wapiga kura wake wamesahau na kwenda mahakamani ni kuonesha anawajali wapiga kura wake. HATA MIMI NISINGEMUELEWA WENJE NA NINGEANZISHA BIFU NAE
   
 18. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mutakyamirwa, swali lako is a million dollar question... hali hiyo inalenga kuminya haki ya wanyonge, ni dalili nyingine ya mfumo fisadi. Wanasheria karibuni
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mutakyamirwa,

  Sheria ya kuweka dhamana ni kandamizi. Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho na kutoa nafasi ya mlalamikaji kuiomba mahakama ipunguze kiasi hicho au asilipe kabisa baada ya kutoa sababu kwamba hana uwezo. Hapo kuna udhaifu. Kwanza inakuwa kama adhabu kwa mlalamikaji. Kigezo kwamba mtu anauwezo hivyo alipe sio sahihi. Ingekuwa na maana kama kigezo kingekuwa chance to succeed. Kama uwezekano wa kushinda ni mdogo mtu asipunguziwe kama ni mkubwa apunguziwe.
   
Loading...